Tuesday, March 11, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14.
Do you like this story?
Jumla
ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa
nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo
tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III
A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za
sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).
Orodha
rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa
kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz)
na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo
tarehe 15 Machi, 2014.
Walimu
wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa
ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.
Inasisitizwa
kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi
na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili
2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza
ajira.
Mwalimu
yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi
zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.
Ikumbukwe
kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa
mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli
ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango
vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao.
Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.
Ofisi
ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi
walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu
kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.
Ni
vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao
tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na
hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao na
kuendelea na kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14.”
Post a Comment