Wednesday, March 19, 2014

MTUHUMIWA WA MAUAJI AJINYONGA KITUO CHA POLISI.





MAHABUSU aliyefahamika kwa jina la Nasson Paul (70) mkazi wa Ruiwa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya  amejinyonga na kupoteza maisha akiwa ndani ya mahabusu.

Akielezea tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi  amesema tukio hilo limetokea machi 18 mwaka huu  majira ya saa 04:50 alifajili  asubuhi katika mahabusu ya polisi  iliyopo kituo cha Kati cha  Mbeya mjini.

Amesema, marehemu huyo alipoteza maisha muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya kupatiwa matibabu..

Msangi, akifafanua kutokea kwa tukio hilo, amesema marehemu huyo akiwa ndani ya chumba chake cha mahabusu inadaiwa alifanya jaribio la kujinyonga kwa kutumia shati lake.

Amesema, akiwa katika harakati hizo za kujiua baadhi ya askari wa zamu aliingia ndani ya chumba hicho ikiwa ni moja ya utaratibu wao wa kukagua na kushuhudia mwili wa mzee huyo ukiwa chini huku akipumua kwa shida.

Amesema, askari hao walimchukua marehemu akiwa  katika hali mbaya kwani alikuwa haongei na kumkimbiza hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.

Hata hivyo,  Kamanda huyo, amesema kuwa marehemu alikuwa akikabiliwa na kosa la  mauaji na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya

0 Responses to “MTUHUMIWA WA MAUAJI AJINYONGA KITUO CHA POLISI.”

Post a Comment

More to Read