Wednesday, March 19, 2014

WANAFUNZI WAMKATA PANGA MWALIMU WAO.




Wanafunzi wawili wa shule ya sekondari  ya kibara, wilayani bunda  wamefikishwa  mbele ya mahakama  ya hakimu mkazi  wa bunda wakikabiliwa  na shtaka l a kumshambulia na kumjeruhi kwa panga mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Ilielezwa  kuwa wanfafunzi hao walimjeruhi  mwalimu huyo  baada ya kutaka kurejeshewa fedha zao za ada kwa vile hawakuwa na mpango  tena wa kuendelea na masomo  shuleni hapo.

Hata h ivyo imeelezwa kuwa  kuna uongozi wa shule  hiyo ulipnga azma hiyo  ya wanafunzi kuacha shule  na kurejeshewa  fedha zao.

Mwendesha mashataka mkaguzi msaidizi wa polisi masoud Mohamed aliwataja washtakiwa hao  wanaosoma kidato cha tatu kuwa ni amosi shirima (22) na james athuman (22)

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo machi 17 mwaka huu.

Mohammed alidai kuwa siku ya tukio saa 5:00 asubuhi  washtakiwa  hao kwa pmoja walimvamia mkuu wa shule aliyotajwa  kwa jina la awadh said  wakati akiwa ofisini kwake shuleni hapo.

Baada ya kuvamia ofisini kwake watuhumiwa walimshambulia  sehemu mbali mbali za mwili  kwa panga na kusababisha majeraha makubwa.

Masoud alisema baada ya wmalimu kuona ashambulia alipiga kelele  za kuomba msaada kabla ya watu kujitokeza  na kuwakamata  watuhumiwa na baadaye kuwapeleka kituo cha polisi .

Washtakiwa  kwa pamoja wamekana shtaka  lao mbele ya  hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo safina semfukwe.

Hakimu semfukwe aliamuru washtakiwa  kurudishwa rumande mpaka kesi yao itakapotajwa  april mosi 2014.


0 Responses to “WANAFUNZI WAMKATA PANGA MWALIMU WAO.”

Post a Comment

More to Read