Wednesday, March 19, 2014

MARIDHIANO YAMRUHUSU WARIOBA KUHUTUBIA.




Mtafaruku ulioibuka  juzi bugeni na kusababisha kusitishwa kwa kikao bila mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji joseph warioba kuwasilisha rasimu ya kativa ulihitimishwa kwa maridhiano  baada ya mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Samuel sitta kukutana na viongozi wa umoja wa katiba  ya watanzania (ukawa) juzi usiku.

Baada ya maridhiano hayo sitta aliliambia bunge jana kwamba alilazimika kufuta baadhi ya semina za masuala ya uelewa kuhusu muungano ambao zipaswa kufanyika na kubakiwa na moja tu ya kupata uzoefu wa Kenya ambayo itatolewa kesho na magwiji wa katiba wan chi hiyo ikiwamo aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya kativa nchi hiyo amos wako.

Juzi baadhi ya wajumbe wa bunge hilo walimzuia jaji warioba kwa makelele kugonga meza wakidai kuw sitta alikuwa amekiuka kanini kwa kumwalika warioba kuwasilisha rasimu ya katiba kabla ya Rais Kikwete kulifungua bunge.

Pia walidai kuw kulikuwa na semina zilizokuwa zimeandaliwa kinyume na kanini ambazo zingewezesha   kuigizwa  misimamo  ya baadhi ya vyana na kwamba jaji warioba alikuwa amepangiwa muda mfupi kinyume na ukubwa wa kazi aliyokuwa nayo . awali ilipangwa  kuwa wajumbe wapate semina ya kijifunza zaidi kutoka kwa wakongwe juu ya masuala ya muungano Na historia ya nchi mbili za tanzangika na Zanzibar.

Waliotarajiwa kutoka semina hiyo ni ramadhani mapuri na wadil kavishe kutoka Zanzibar wakati kwa upande wa bara walialikwa Hassan ngwilizi na profesa issa shivji.

0 Responses to “MARIDHIANO YAMRUHUSU WARIOBA KUHUTUBIA.”

Post a Comment

More to Read