Wednesday, March 19, 2014

SHIBUDA AMWANGUKIA JK KUHUSU MUUNGANO.




Rais Jakaya Kikwete, ameombwa katika hutuba yake ya kuzindua Bunge la Katiba, atoe msimamo wake juu ya Muundo wa Muungano, badala ya kuwa na msimamo wa makundi ya kisiasa.
Akizungumza na Mwananchi, Mjumbe wa Bunge la Katiba, John Shibuda, alisema hivi sasa ni muhimu  kila kiongozi kutoa msimamo wake na maoni katika masuala ya msingi.

“Tunatarajia rais atambulishe maoni yake, katika kulitakia mema Taifa na kutoa mwelekeo wa taifa, “ alisema Shibuda.
Rais Jakaya Kikwete anatarajia kulizindua Bunge la Katiba Ijumaa wiki hii katika mazingira ambayo Bunge lenyewe limegawanyika kimtazamo kuhusu mambo makuu mawili; upigaji kura na Muungano wa  Tanzania. Wakati Chama Tawala CCM kikitaka kura zipigwe kwa uwazi na muundo wa Muungano uwe wa serikali mblli, wapinzani wanataka kura zipigwe kwa siri.

Hata hivyo wapinzani wamegawanyika kuhusu Muungano wa Tanzania ambapo, Chadema wanataka Muungano wa Serikali tatu na CUF Serikali ya mkataba.

Katika hatua nyingine Shibuda amesema binafsi katika muundo wa Muungano, anaunga mkono serikali mbili. Nitatetea msimamo huo popote na wakati wowote, anasema.

“Katika Bunge hili mimi nitakuwa natoa msimamo kwa kila ambacho nakiamini na siyo kufuata makundi ya watu,” amesema Shibuda.

0 Responses to “SHIBUDA AMWANGUKIA JK KUHUSU MUUNGANO.”

Post a Comment

More to Read