Tuesday, March 18, 2014
WAZEE WA YANGA WASITISHA MAANDAMANO YAO.
Do you like this story?
Baraza la wazee wa Klabu ya Yanga, leo limetoa tamko
la kusitisha maandamano yao ambayo walikuwa wameyapanga kufanyika ili
kushinikiza serikali kutoa kibali cha Ujenzi wa uwanja wao wa kisasa
unaotarajia kujengwa sehemu ya Jangwani, Dar es Salaam.
Tamko
hilo la kusitisha maandamano hayo limetoleo mara baada ya baadhi ya viongozi wa
juu wa timu hiyo kukutana na viongozi wa serikali.
Viongozi hao wa serikali walitoa tamko
kuhusu kushughulikia ombi lao hali iliyosababisha viongozi wa Yanga kusitisha
maandamano yao waliyokuwa wameyapanga kuyafanya juma hili.
Juma lililopita Katibu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali alitoa siku tano kwa Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala, liwe limewapa kibali cha ujenzi huo, vinginevyo waliahidi kufanya maandamano makubwa.
Amesema viongozi wa juu wa klabu hiyo walikutana na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik, Meya wa Ilala Jery Silaa na Diwani wa Kata ya Jangwani ambapo walikubaliana ombi lao kufanyiwa kazi.
Akilimali amesema serikali kupitia
Manispaa ya Ilala ilieleza kuwa ombi lao linashughulikiwa kwa haraka, hivyo
aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuelewa jambo hilo bila kuwepo na migogoro.
Ameweka wazi kuwa wanaamini serikali kupitia Manspaa ya Ilala watalishughulikia ombi lao, ingawa amesisitiza kuwa ikitokea ombi lao hilo linaloshughulikiwa likija na majibu ya “hapana” watatafuta mbinu nyingine.
"Sisi tumeomba hivyo majibu ni mawili ndiyo tumepata au tumekosa, ikitokea likaja jibu la kukosa hapo ndiyo kutakuwa na utata na kuamua cha kufanya," alisema katibu huyo wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga.

Ameongezea kuwa klabu hiyo imejiandaa
kuwalipa watu waliongezeka katika eneo lao, hivyo hawaoni sababu za kwenda
kujenga nje ya mji wakati wao ni watoto wa mjini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZEE WA YANGA WASITISHA MAANDAMANO YAO.”
Post a Comment