Saturday, May 20, 2017
Full Ripoti: Jeshi la Polisi Pwani labaini mtandao wa watuhumiwa wa mauaji Kibiti.
Do you like this story?
Picha za watuhumiwa wa mauaji wanaosakwa Pwani
JESHI
la polisi mkoani Pwani ,limewabaini baadhi ya mtandao wa watuhumiwa wa
mauaji yanayoendelea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji wapatao kumi na
mbili akiwemo mwanzilishi wa mauaji Abdurshakur Ngande Makeo .
Aidha jeshi hilo linaendelea na msako kuwatafuta watu hao ambao wanne picha zao zimepatikana .
Akizungumzia
hali ya kiusalama ya Mkoa kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea
katika wilaya hizo ,Kamanda wa polisi mkoani hapo,Onesmo Lyanga
,alisema wanaendelea na mapambano na upelelezi kuwapata wahusika wote .
Alieleza jeshi la polisi limewabaini kwa majina na picha kwa baadhi yao.
Kamanda
Lyanga ,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faraj Ismail Nangalava ,Anaf
Rashid Kapera @Kapelo ,Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa .
Wengine
ni Shaban Kinyangulia ,Haji Ulatule ,Ally Ulatule ,Hassan Uponda
,Rashid Salim Mtulula ,Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame .
Kamanda
Lyanga ,alieleza kwamba ,Saidi Ngunde inadaiwa anaishi Ikwiriri na Omar
Abdallah Matimbwa anaishi Dar es salaam ambapo picha zao wanazo pamoja
na ya Faraj na Anaf .
Alieleleza
wengine nane bado picha zao hazijapatikana hadi sasa .“Jeshi letu
limebaini hayo kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na
uchunguzi zaidi ” alibainisha .
Kamanda
Lyanga alisema ,watuhumiwa hao ,wamegundulika kuwa hupendelea
kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga ,kisiwa cha Saninga kijiji
cha Nchinga .
Kamanda
huyo ,alifafanua kijiji kingine ni cha Mfesini kata ya Nyamisati na
maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti ,Rufiji na Mkuranga.
Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa siri kufichua watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama kimkoa.
Limetangaza bingo ya kumpatia sh. mil .tano yeyote atakaefanikisha zoezi hilo .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)