Saturday, May 20, 2017
Kutana na Mama aliyejifanya mwanaume ili afanye kazi mgodini
Do you like this story?
Pili
Hussein alitamani kujiimarisha kimaisha na mawe ya thamani
yanayosemekana kuwa nadra mara elfu mia moja kuliko almasi, lakini kwa
kuwa wanawake hawakuwa wanaruhusiwa kwenye migodi hiyo alivalia mavazi
kama mwanamume na kuwadanganya wafanyikazi wenzake kwa zaidi ya mwongo
mmoja.
Pili
alilelewa katika familia kubwa mjini Tanzania. Mtoto wa mchugaji ambaye
aliyekuwa na mashamba makubwa, babake Pili alikuwa na wake sita na
alikuwa miongoni mwa watoto 38.
Licha ya hayo yote alilelewa vyema kwa njia tofauti.
''Babangu alinichukulia kama mwanamume na nilikuwa nikichunga mifugo yake, lakini sikuyapenda maisha hayo kabisa'', alisema.
Hata ndoa yake haikuwa ya furaha, akiwa na umri wa miaka 31 Pili aliikimbia ndoa yake iliyokumbwa na migogoro ya kinyumbani.
Alipokuwa akitafuta ajira alijipata katika mji mdogo wa Mererani, Tanzania, uliopo chini ya mlima mkuu wa Kilimanjaro.
Eneo hilo ni maarufu sana duniani kwa kuwa na madini nadra ya rangi ya samawati ya tanzanite.
''Sikwenda shule , kwa hivyo sikuwa na mambo mechi kuchagua,'' Pili alisema.
''Wanawake
wahakuruhusiwa kwenye maeneo ya migodi hiyo, nikajitosa kama mwanamume
shupavu na mwenye nguvu. Nilichukua suruali ndefu na kuzikata zikawa
kama kaputula ili kufanana na mwanamume. Hivyo ndivyo nilivyofanya.''
Ili kukamilisha mabadiliko yake , alibadilisha pia jina lake.
''Niliitwa Uncle Hussein {akimaanisha mjomba Hussein}, sikumwambia yoyote kuhusiana na jina langu halisi la Pili.
Hata leo ukija katika kambi hiyo utanitafuta kwa jina hilo la Uncle Hussein.''
Kwenye
migodi hiyo yenye joto ,uchafu mwingi na wenye kina cha mita mia moja
chini ya ardhi Pili angefanya kazi kwa saa 10-12 kwa siku , akilima na
kuchunga akiwa na matumaini ya kupata mawe hayo ya thamani kwenye
mishipa ya mawe hayo ya grafiti.
''Ningeenda hadi mita 600 chini ya mgodi, mara kwa mara nikiwa shupavu kuliko wanaume wengine.
Nilikuwa na nguvu nyingi na niliweza kufanya kazi kama matarajio ya wanaume wengine wangefanya.''
Pili amesema hakuna aliyemshuku alikuwa mwanamke.
''Nilijifanya kama nyani aina ya Gorilla'' alisema, Nilipigana, lugha yangu ilikuwa mbaya , nilibeba kisu kikubwa kama Maasai.
Hakuna mtu alifahamu kwamba mimi ni mwanamke kwa sababu kile nilichokuwa nikifanya nilikifanya kama mwanamume.''
Baada
ya mwaka mmoja, alipata utajiri , alipopata mawe mawili makubwa ya
Tanzanite. Kutokana na pesa alizozipata alimjengea babake, mama na pacha
wake nyumba mpya na akajinunulia vifaa zaidi na akaanza kuajiri
wachimba migodi kumfanyia kazi.
Na kujificha kwake kuliwashawishi kwamba alichukua hatua zisizo za kawaida kwa utambulisho wake kujulikana.
Mwanamke mmoja aliripoti kwamba alikuwa amebakwa na wachimba migodi Pili akiwa miongoni mwa washukiwa.
''Polisi
walipokuja, wanaume waliotekeleza ubakaji huo wakasema: 'Huyu ndio
mwanamume aliyetekeleza hilo'' na nilipopelekwa katika kituo cha polisi ,
Pili akasema alikuwa hana namna bali kutoboa siri yake.''
''Aliwauliza
polisi kumleta polisi mwanamke ili amchunguze kwamba yeye hakutekeleza
kitendo hicho na baadaye aliachiliwa huru. Hata baada ya hilo wachimba
migodi wenzake waliona vigumu kuamini walikuwa wamedanganyika kwa siku
nyingi''.
''Hawakuamini
hata polisi waliposema kwamba alikuwa mwanamke," alisema, ''haikuwa
rahisi kwao kukubali hadi mwaka 2001 nilipoolewa na nikaanza familia.''
Kutafuta bwana wakati kila mtu amenizoea kama mwanamume haikuwa rahisi, Pili alipata bwana na akafanikiwa.
Swali lililokuwa akilini mwake lilikuwa,'je ni mwanamke kweli?'' anakumbuka. ''ilimchukua miaka mitano ndipo aliponikaribia.''
Pili
aliikuza taaluma yake na hivi leo anamiliki kampuni yake ya migodi
ambayo ameajiri wachimba migodi 70 , watatu kati yao ni wanawake, lakini
wanafanya kazi ya upishi.
Pili
amesema licha ya kwamba kuna wanawake wengi katika makampuni ya migodi
kuliko wakati wake, hata leo ni wanawake wachache wanaofanya kazi kwenye
migodi hiyo.
''Wanawake
wengine huyaosha mawe hayo , wengine ni wakala na wengine ni wapishi'' ,
alisema, ''lakini hawaingii ndani ya migodi , si rahisi kumpata
mwanamke akifanya nilichofanya wakati wangu.''
Mafanikio
ya pili yamemuezesha kuwalipia karo watoto wa ndungu zake 30 na
wajukuu. Licha ya hayo amesema hawezi kumrai mwanawe kufuata nyayo zake.
''Najivunia kwa kile nilichokifanya, imenifanya tajiri lakini ilikuwa vigumu kwangu'', amesema.
''Nataka
kuhakikisha mtoto wangu ataenda shule apate elimu na ataweza
kujiendeleza kimaisha kwa njia tofauti mbali na nilivyopitia.''
Subscribe to:
Post Comments (Atom)