Tuesday, April 8, 2014
ALIYEKUWA AKIISHI KWENYE HANDAKI JIRANI NA MLIMANI CITY AONDOLEWA NA ASKARI, HANDAKI LACHOMWA MOTO.
Do you like this story?
CHACHA
Makenge (38) aliyeripotiwa awali kuishi ndani ya handaki katika eneo la pori la
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, amepatwa na balaa jipya baada
ya makazi yake kuvamiwa na askari, kukamatwa na mwishowe kupelekwa Muhimbili
kitengo cha wagonjwa wa akili kwa ajili ya matibabu.
Kana
kwamba haitoshi, Makenge ambaye aliwahi kuishi katika handaki hilo kwa muda wa
miaka mitano, alipotoka, alikuta makazi yake hayo yakiwa yamechomwa moto na
vitu vyake vyote kuchukuliwa.
Akizungumza
na gazeti hili, kijana huyo alikiri kutokewa na mambo hayo na kulalamika kuwa
kitendo alichofanyiwa, kimempotezea mwelekeo wa maisha yake kwani hana tena
sehemu ya kwenda kwa kuwa hakujiandaa.
Alisema
alipokamatwa alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kudhaniwa kuwa ni
mgonjwa wa akili, lakini alipingana na madai hayo, licha ya kuwa aliishi kwa
siku 36 hospitalini hapo kabla ya kuruhusiwa kuondoka.
Mmoja
wa maofisa wa ulinzi wanaolinda chuoni hapo, Mussa Nakuwa aliyeendesha
oparesheni ya kumkamata kijana huyo, alisema vifaa vyake vyote vilipelekwa
Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kuhifadhiwa na
anaweza kwenda kuvichukua wakati wowote.
Habari
zingine kuhusiana na mtu huyo zinadai amechimba mahandaki mengine kadhaa ya
siri ambayo anayatumia kwa ajili ya kulala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ALIYEKUWA AKIISHI KWENYE HANDAKI JIRANI NA MLIMANI CITY AONDOLEWA NA ASKARI, HANDAKI LACHOMWA MOTO.”
Post a Comment