Saturday, May 3, 2014

OWEN: `HAKUNAGA` KAMA CRISTIANO RONALDO REAL MADRID.



Michael Owen enzi zake akiwa Real Madrid


MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa England, Michael Owen anaamini Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji mkubwa zaidi kwa wakati wote katika klabu ya Real Madrid.

Ronaldo amekuwa katika kasi kubwa msimu huu na kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa UEFA baada ya kupiga mawili katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bayern Munich katikati ya wiki hii na kufikisha magoli 16.

Owen aliyeichezea Real Madrid msimu wa 2004-05 amevutiwa na kiwango cha Ronaldo na kuthubutu kusema kwasasa nyota huyo ni tunu ya klabu zaidi ya Ferenc Puskas.

“Nadhani mchezaji mkubwa zaidi kwa wakati wote Real Madrid ni Cristiano Ronaldo akifuatiwa na Ferenc Puskas”. Owen ameandika katika kolamu yake kwenye gazeti la Sportlobster .

“Ronaldo amelingana na Puskas” . amekuwa na rekodi kubwa ya mabao 242 katika mechi chache.
“Pia amekuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga mabao 100 kwa haraka zaidi na ameshikilia rekodi ya kuifungia Madrid mabao mengi zaidi ndani ya msimu mmoja”.

Pia kwa kifupi, Owen alielezea maisha yake alipokuwa Real Madrid kuwa yalikuwa mazuri kwa kazi yake hasa kwa vyombo va habari na mashabiki wake.
“Sikuwa na wasiwasi ya kutopata mafanikio katika uwanja maarufu.

“Nilikuwa na mambo mawili: Nitafanya nini nitakaposhika mpira kwenye utambulisho wangu Santiago Bernabeu na pili nitakaa wapi katika vyumba vya kubadilishia nguo”.
“Nilikuwa katika wasiwasi mkubwa wakati wa utambulisho”.
“ Nilikuwa nafirikia maujanja ya kufanya nitakapotupiwa mpira.
“Nilionesha ufundi mkubwa mbele ya vyombo vya habari na mashabiki waliokuwepo Bernabeu”.
“Hakukuwa na jinsi ya kushindwa mbele ya vyombo vya habari vya dunia”.
Ghafla Owen aliondoka Madrid ndani ya msimu mmoja akifunga mabao 14 tu katika mechi 36 za La Laiga alizocheza.

0 Responses to “OWEN: `HAKUNAGA` KAMA CRISTIANO RONALDO REAL MADRID.”

Post a Comment

More to Read