Saturday, May 3, 2014
2000 WAFUKIWA KWA UDONGO AFGHANISTAN.
Do you like this story?
Juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili Kaskazini mashariki mwa
Afghanistan ambapo watu wapatao elfu mbili wanasadikiwa kufa kutokana na
maporomoko ya ardhi katika maeneo ya vijiji kwenye mkoa wa Badakhshan.
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa wa karibu mita kumi
kwenda juu baada ya sehem ya mlima mmoja kuporomoja kutokana na mvua kubwa
zinazonyesha.
Miili ya watu wapata 350 imepatikana hapo jana katika maporomoko ya
ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana
akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 4000 hawana makazi.
Mashirika ya misaada na uokoaji kwa sasa wameanza kuwapa mikate na maji
maelfu ya watu waliolala nje kwenye baridi kali wakiwa hawana makazi.
Kuna taarifa nyingine zinazosema maelfu mengine ya watu huenda wakawa
wametoweka baada ya upande mmoja wa mlima kuangukia kijiji k katika eneo la
mashambani la mkoa wa Badakhshan unaopakana na mataifa ya Tajikistan,Uchina na
pakistan.
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka
manusura.
Mwandishi wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo hilo ni miongoni mwa
maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa maskini duniani na huenda
ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali kubaini ukubwa wa janga hilo.CHANZO
BBC SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “2000 WAFUKIWA KWA UDONGO AFGHANISTAN.”
Post a Comment