Saturday, April 26, 2014
CHUO KIKUU MZUMBE CAMPUS YA MBEYA WAUNGANA NA WATOTO YATIMA NCHINI KUSHEREKEA SHEREHE ZA MUUNGANO.
Do you like this story?
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Campus
ya Mbeya Prof.Kihanga Ernest mwenye Suti Nyeusi akiwa na Mwadhiri Ladslausi Rwekaza wakiwa wanateta jambo.
|
Profesa Kihanga akizungumza na
baadhi ya watoto hao kabla ya kukabidhiwa msaada kwa mama malezi wa kituo hicho.
|
Mama mlezi Bi Anna Kasile wa kituo cha watoto yatima kilichopo Simike Mkoani Mbeya akitoa maelezo |
Baadhi ya wanajumuiya hao
wakikabidhi msaada kwa mama mlezi wa kituo hicho Bi.Anna Kasile.
|
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Campus ya Mbeya Prof.Kihanga Ernest Akiwa na Steven john mwadhiri wakikabidhi kiasi cha pesa shillingi Laki Tano(500,000) pamoja na vitu Mbalimbali. |
Jumuiya ya
Chuo Kikuu Mzumbe Cumpus ya Mbeya imeungana watoto yatima Mkoani Mbeya na
Baadhi ya maeneo Mengine Nchini Katika Kusherekea Kilele cha Sherehe za
Muungano.
Jumuiya hiyo
ambayo ni mchanganyiko wa wanafunzi walimu na watumishi wote wa chuo
hicho wameungana kwa pamoja na kutoa msaada wa chakula pamoja na mahitaji mengine
katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Malezi ya Huruma kilichopo Simike
jijini Mbeya msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi mil2.
Akikabidhi
Msaada huo kwa niaba ya wanajumuiya hao Mkuu wa chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya
Prof.Kihanga Ernest amesema hatua ya kutimiza miaka 50 ya muungano wa Tanzania
ni furaha kubwa hivyo wao wameamua kufurahi na watoto wanaoishi katika
mazingira magumu.
Amesema
isingekuwa vyema kusherekea sherehe hizo wakati kuna watu wanaishi katika
mazingira magumu na wanahitaji msaada kwa mahitaji mbalimbali hivyo
msaada huo ni sehemu ya kuifanya jamii kama hiyo kuwa kwa pamoja katika sherehe
hizo.
Hata hivyo
profesa huyo amesema katika muungano huo umekuwa na amani kubwa sana hivyo hata
vijana hao wanapaswa kufurahi na kuiona faida hiyo ili nao waweze kujua
historia na hatimaye kuendelea kuulinda muungano huo.
Pamoja na
muungano huo kudumu kwa miaka 50 lakini pia umetoa fursa kwa vijana kupata
elimu Uzanzibari na Utanganyika pamoja na kuitangaza vyema Tanzania
Kimataifa kama sehemu ya Amani .
Aidha
Profesa huyo amelitaka bunge la katiba kuangalia kwa umakini suala
kuulinda muungano huo kwa kuhakikisha linaingia katika Katiba mpya.
Aidha Kwa
upande wake Mratibu wa shughuli hizo ambaye pia ni Mhadhiri wa chuo hicho Ndugu
Steven John amesema kuwa tofauti na kusherekea miaka 50 ya Muungano
lakini pia wameona washilikiane na jamii ili isionekane kuwa chuo kikuu ni
sehemu ya kusoma tu badala yake iwe sehemu ya jamii.
Amesema
wameamua kuonyesha mjumuiko wao na watu wanaowahitaji ili kuweza
kuleta nuru ya siku ya muungano kwani wanaamini yapo mengi wanayohitaji lakini
kwa kufanya hivyo kutaleta faraja kubwa kwa kundi hilo.
Amesema
msaada uliotolewa na wanajumuiya hao ni michango toka katika mifuko yao binafsi
bila kuhusisha taasisi hiyo ya Mzumbe .
Akipokea
msaada huo Mama mlezi wa kituo hicho Ndugu Anna kasile amesema msaada
uliotolewa na wanajumuiya hao umefika katika siku muafaka hasa kutokana na
kuwepo kwa uhaba wa chakula katika kituo kilichopo Morogoro ambacho nacho kipo
chini yake.
Amesema
msaada huo utagawanywa ambapo chakula kingine kitasafirishwa na kupelekwa
mkoani morogoro hivyo amewashukuru wanajumuiya hao kwa kuonyesha moyo huo.
Amesema
katika kituo hicho cha Simike kinajumla ya watoto 120 ambao wanahitaji gharama
kubwa katika kuwahudumia hivyo msaada huo unawasaidia kwa kiasi kikubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CHUO KIKUU MZUMBE CAMPUS YA MBEYA WAUNGANA NA WATOTO YATIMA NCHINI KUSHEREKEA SHEREHE ZA MUUNGANO.”
Post a Comment