Saturday, April 26, 2014
KUNUSURIKA KUPOROMOKA DARAJA KWAWAPA SOMO PRISONS.
Do you like this story?
MAAFANDE wa Tanzania Prisons `Wajelajela`
wanasubiri kwa hamu kubwa ripoti ya kocha wao, David Mwamwaja ili waanze
kuandaa mikakati mapema kuelekea msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania
bara.
Katika mahojiano maalum na Mtandao huu, Katibu
mkuu wa Prisons, Inspekta Sadick Jumbe amesema misimu miwili mfufulizo wamenusurika
kushuka daraja, hivyo malengo yao ni kusajili wachezaji wazuri ili msimu ujao
washeka nafasi tano za juu.
“Sisi ni viongozi
na tuna majukumu yetu. Tumeona makosa yetu, lakini inapofika mambo ya
ufundi, Mwamwaja ndiye mwenye majukumu”.
“Tuna imani na kocha huyo mwenye historia kubwa
katika soka. Anaandika ripoti yake ambayo tutaipata ndani ya wiki moja ijayo”.
“Kwa kufuata mapendekezo yake, sisi viongozi
tutatekeleza kila alichokiona na kumshauri kwa yetu machache tuliyoyaona kwa
nafasi ya viongozi”. Alisema Jumbe.
Pia Jumbe alisema timu za majeshi zimeonakana kuwa
dhaifu mno msimu huu na moja ya sababu ni kukosa maandalizi mazuri na masuala
ya kiuchumi.
“Angalia kule chini wamemaliza Rhino, Oljoro pale juu
yao amekuja Ashanti timu ya kiraia, halafu Mgambo na unatukuta sisi Prisons”.
“Kinachotuathiri sisi ni maandalizi duni na uhaba
wa fedha”.
“Pia aina ya wachezaji tulionao. Sisi tunachukua
raia, wakifika wanajituma sana, lakini wakiwa maaskari wanaona sasa mpira sio
kazi tena”
“Kinachozibeba timu za kiraia ni wachezaji
kutambua kuwa mpira ni kazi yao na wakifanya vibaya watakosa kwa kwenda. Lakini
kwetu ni tofauti kabisa”.
“Vijana wamekuwa wazembe sana hususani wanapopata
kazi kwasababu wanajua wakishuka daraja, wataendelea kupata mshahara kwa kazi
yao ya uaskari”. Alisema Jumbe.
Jumbe aliongeza kuwa timu za majeshi zinaonekana kutokuwa na mvuto
kwa mashabiki wengi wa soka kwasababu ya aina ya kazi yao.
“Sisi maaskari ya magereza, kazi yetu ni kutunza
wahalifu. Angalia Polisi kazi yao ni kushika wahalifu. Hali hii imezitenganisha
timu na waanchi”.
“Kwa mfano mtu akisikia Mbeya City fc anaona ni
timu yake, lakini akisia Tanzania Prisons anaona kama timu ya Tanzania nzima.
Hapana! Prisons ipo Mbeya na kila kitu kinafanyika Mbeya”
“Ili kuhakikisha tunairudisha timu kwa wananchi,
Prisons tumefungua matawi maeneo tofauti.
“Tuna matakiwa Uyole, Mwanjelwa, Mabatini, Sinde,
Isanga na maeneo mengi.”
“Matawi yapo maeneo mengi, angalia mechi yetu ya
mwisho na Ashanti United. Mashabiki walisafiri kutoka matawini na kuja
Morogoro. Tunawakaribisha watu waje kujiunga na Prisons”. Alisema Jumbe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUNUSURIKA KUPOROMOKA DARAJA KWAWAPA SOMO PRISONS.”
Post a Comment