Saturday, March 15, 2014

KERO:WACHUUZI WA MBOGAMBOGA NA MATUNDA SOKO LA NONDE ITIJI JIJINI MBEYA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA UKOSEFU WA VYOO.


Soko la Itiji wachukuzi wakiwa wanaandaa biashara zao nyakati za asubuhi


Biashara zikiendelea nyakati za mchana.


Hivi ni vyoo vinavyo tumika na wafanyabiashara wa sokoni hapo

Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Itiji


Afisa Mtendaji kata ya Itigi Ndugu Leonard Magoma

Afisa Mtendaji kata ya Itigi Ndugu Leonard Magoma ambaye naye kwa upande wake amekili kuwepo kwa hali hiyo ambapo amedai kuwa chanzo kikubwa cha kuharibika kwa vyoo katika soko hilo unatokana na baadhi ya watu kuiba milango ya vyoo hivyo pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo.



Amesema pamoja na ubovu wa miundombinu katika soko hilo lakini pia soko hilo halipo rasmi kama masoko mengine licha ya Halmashauri ya jiji kuendelea kuchukua ushuru wa shilingi mia mbili kwa kila meza huku akidai kuwa watu wanao fanya biashara katika eneo hilo wanatambua  kabisa kuwa soko hilo sio rasmi kwa shughuli za kisoko.


Amesema kwa sasa mipango iliyopo ni kuwatoa watu hao na kuwapeleka eneo jingine ambalo tayari limekwisha tengwa kwa ajili ya shughuli hizo za soko kwani mipango ya halimashauri ni kuwaondoa watu hao na kuweka Kituo cha Afya .
.

Amesema pamoja na kuwepo kwa mipango ya kuboresha hali ya soko hilo lakini pia ametoa lawama  kwa wajasilimali hao kwa kudai kuwa hata wao kwa upande wao wanahusika na usafi wa mazingira sokoni hapo licha ya kwamba halimashauri ya  jiji kuwa ndio muhusika mkuu wa usafi katika eneo hilo.

Amedai kuwa hata wao  pia wanauongozi wao ambao unaweza kuratibu shughuli za usafi na utunzaji  wa mazingira sokoni hapo badala ya kulalamikia mamlaka husika kuwa zimeshindwa kuboresha usafi katika eneo hilo.

Jumla ya wachuuzi 1000 wa mbogamboga na matunda wanatumia soko hilo ambalo kwa sasa lipo katika hatari ya kutokea kwa magonjwa ya mlipuko hivyo juhudi za haraka zinahitajika ili kuokoa hali hiyo




0 Responses to “KERO:WACHUUZI WA MBOGAMBOGA NA MATUNDA SOKO LA NONDE ITIJI JIJINI MBEYA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA UKOSEFU WA VYOO.”

Post a Comment

More to Read