Sunday, May 18, 2014
WENGER BAADA YA KUBEBA `NDOO` YA FA ASEMA HANG`ATUKI ASERNAL
Do you like this story?
Haondoki: Bosi wa Asernal, Aserne Wenger amethibitisha kuendelea kuwepo klabuni hapo |
Pati: Lukas Podolski akimlowesha kwa bia bosi wake, mzee Wenger baada ya kombe la FA |
Aogeshwe huyoo: Wenger akiwa amebebwa na kumwagiwa bia na wachezaji wake.
|
Kutoka kushoto ni Santi Carzorla, Mesut Ozil, Per Mertesacker, Serge Gnabry, Lukas Podolski na Aaron Ramsey |
KOCHA wa Arsenal, mfaransa, Arsene Wenger sasa
anatarajiwa kusaini mkataba mpya baada ya kufuta ukame wa miaka 9 bila kombe
kufuatia kutwaa ndoo ya FA jana kwa kuwanyuka 3-2 Hull City katika mechi ya
fainali iliyopigwa dimba la Wembley.
Wenger alisema jambo la kusaini mkataba litafanyika
kwasababu yeye na bodi ya timu wapo katika mazingira mazuri.
“Kamwe sijiulizi kuondoka zaidi ya kujiuliza nini
klabu yangu ifanye”. Alisema Wenger.
Wenger amekaa Asernal bila kombe kwa siku 3, 283
sawa na miaka 9 na kucheza mechi 512, lakini jana alijifuta machungu pamoja na
mashabiki wa Asernal
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WENGER BAADA YA KUBEBA `NDOO` YA FA ASEMA HANG`ATUKI ASERNAL”
Post a Comment