Sunday, May 18, 2014
KIJANA AFIA KABURINI WAKATI AKIFUKUA KABURI ILI AIBE FUVU LA MAREHEMU,TAZAMA PICHA
Do you like this story?
Maiti ya kijana huyo ikiwa imenasa kaburini |
Tukio la ajabu na la kushangaza limetokea huko
nchini Nigeria baada ya kijana mmoja kukutwa akiwa amekufa kaburini,kijana huyo
alikumbwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la
marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina.
Kwa mujibu wa mtandao wa Saturday Tribune wa
Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo
alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa
kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo
lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi walikimbia na kumuacha
akihangaika kujinasua,lakini jitihada zake ziligonga mwamba mpaka pale
umautiulipo mkuta.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na tope.
Wakazi wa eneo hilo waliripoti polisi na
walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka
nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIJANA AFIA KABURINI WAKATI AKIFUKUA KABURI ILI AIBE FUVU LA MAREHEMU,TAZAMA PICHA ”
Post a Comment