Saturday, May 28, 2016
MBARONI KWA KUKUTWA WAKITOA MAMILIONI KWA ATM ZA WATU 19
Do you like this story?
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa
wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi 3,680,000 wakiwa
na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. .
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu
walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .
Watuhumiwa
hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea,
wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.
Nyanda ameeleza
kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na
kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea fedha .
Amesema
baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa
hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine
za kutolea fedha.
Kaimu
Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na
waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za
siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi cha fedha taslimu
shilingi 3,680,000.
Amezitaja
Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC 61908000058,AC
61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237, AC
61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.
Kaimu
kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba
AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac 61902400818, AC
61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC 70408100131.
Amesema
watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo
kukamilika na bado watuhumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la
polisi kwa mahojiano zaidi .
Kaimu
kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za namba
zao za siri za kadi wanazozitumia kwenye ATM za benki .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MBARONI KWA KUKUTWA WAKITOA MAMILIONI KWA ATM ZA WATU 19”
Post a Comment