Saturday, May 28, 2016

CRISTIANO RONALDO ALILIA MKATABA MPYA REAL MADRID.




KWA kilea ambacho unaweza kusema ni kama kanogewa, straika Cristiano Ronaldo ameitaka Real Madrid kuharakisha kumpa mkataba mpya ili aendelee kubaki Santiago Bernabeu, licha ya kuwepo kwa tarifa zinazomuhusisha kwenda kujiunga na PSG.
 Mkataba wa sasa wa Ronaldo unamalizika mwaka 2018, katika kipindi ambacho Mreno huyo atakuwa na umri wa miaka 33. 

Pamoja na kuwa na umri huo, mfungai bora huyo hajaonyesha kuzeeka ikiwa ni baada ya kufunga zaidi ya mabao 50 katika misimu sita ukiwemo huu na huku leo akiwa bado ana mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Atletico Madrid. Hata hivyo, PSG wanaripotiwa kummezea mate Ronaldo ili aweze kuwa mrithi wa Zlatan Ibrahimovic ambaye anataka kuondoka lakini staa huyo wa Real Madrid anasema anataka kubaki.

 “Nitamalizia soka langu Real Madrid,” Ronaldo aliuambia mtandao wa La Sexta. “Katika kipindi cha miaka 15 nataka niwe na miaka 41 ama zaidi,” alisema nyota huyo. “Tutaangalia kama nitaongezewa muda na litakuwa jambo zuri kama Real Madrid wataongeza mkataba wangu,” aliongeza. “Nataka kubaki mahali hapa, pana mengi ya kukumbukwa mazuri na mabaya. Katika kipindi cha miaka minne sikuwa na furaha laini kwa sasa nina furaha na sioni klabu bora kuliko Real Madrid,” alisema tena.



0 Responses to “CRISTIANO RONALDO ALILIA MKATABA MPYA REAL MADRID.”

Post a Comment

More to Read