Saturday, March 15, 2014

ALIYEKUWA RAIS WA SIERRA LEONE " AL HAJJ KABBAH" AFARIKI DUNIA.


Marehemu AL Hajj Kabbah


Amefariki nyumbani kwake akiwa na miaka 82.Alhaji Ahmad Tejan Kabbah alizaliwa February 16, 1932. Aliongoza Sierra Leone kati ya mwaka wa 1996 hadi 1997 na kisha tena mwaka wa 98 hadi mwaka wa 2007Katika miaka mingi ya utu uzima wake, alihudumu kama mtaalamu wa uchumi na sheria. Alifanya kazi kwa miaka mingi na shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP. Baada ya kujiuzulu kutoka umoja huo mwaka wa 92, alirudi zake nchini Sierra Leone na kujiingiza katika siasa za nchi hiyo

Maisha yake ya siasaMnamo mwaka wa tisini na sita, bwana Kabbah alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama Sierra Leone's People's Party (SLPP) na kuwania urais kwa tikiti ya chama hicho mwaka wa 96.

Katika kinyanganyiro hicho, alishinda na kuwa rais kwa 59% ya kura na kumpiku mpinzani wake mkuu John Karefa-Smart wa chama cha United National People's Party (UNPP) aliyepata 40% tu ya kura.

Kikubwa atakachokumbukwa nacho ni hotuba yake ya kuapishwa mjini Freetown, alipoahidi kumaliza kabisa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, jambo alilotekeleza baada ya kuwa rais.

Bwana Kabbah ni wa kabila la Mandingo kiasilia na ndiye aliyekuwa rais wa kwanza wa kiislamu wa Sierra Leone. Alizaliwa katika kijijji cha Pendembu, wilaya ya Kailahun mashariki mwa Sierra Leone, japo udogoni mwake alikulia mji mkuu wa Free town.

Utawala wa KabbahSehemu kubwa ya uongozi wa Kabbah ilishawishiwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyotokea nchini Sierra Leone kwa muda mrefu, huku akikumbwa na mapinduzi ya muda yaliyofanywa na wanamgambo wa United Front wakiongozwa na Foday Sankoh. Mapinduzi hayo yalim'ngoa madarakani kati ya Mei 97 hadi March 98.

0 Responses to “ALIYEKUWA RAIS WA SIERRA LEONE " AL HAJJ KABBAH" AFARIKI DUNIA.”

Post a Comment

More to Read