Friday, May 2, 2014

NEWS ALERT: WAZIRI NYALANDU AMTIMUA PROFESA SONGORWA MBELE YA WABUNGE KIKAONI.




Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amekasirika kiasi cha kukaribia kumkunja Mkurugenzi (halali) wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kilichofanyika BoT, Dar es Salaam, leo.

Profesa Songorwa alikuwa kwenye ujumbe wa maofisa wa Wizara hiyo walioambatana na Nyalandu kwenda kujibu hoja mbalimbali kwenye Kamati hiyo. Baada ya kuwapo ukumbini, Nyalandu alimuona Profesa Songorwa na kumuuliza kaingia ukumbini hapo kama nani. Mara moja, akiwa amehamaki, akaamuru Profesa Songorwa atoke nje. Naye bila ubishi, alitii.


Hata hivyo, baadhi ya wajumbe walipinga hatua hiyo, lakini kama ilivyotarajiwa, na kama mtakanyoendelea kushuhudia, Mwenyekiti wa Kamati, James Lembeli, akaonesha urafiki wake kwa Nyalandu. Akabariki kufukuzwa kwa Songorwa, na kuamuru kikao kiendelee. Baadhi ya wajumbe waliendelea na msimamo wa kupinga kitendo hicho wakisema ni cha udhalilishaji kwa Profesa Songorwa na pia ni dharau kwa mamlaka iliyomrejesha Profesa huyo kwenye nafasi yake.


My take: Mgogoro wa kweli ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii ndiyo kwanza umeanza rasmi. Wapo watakaotumia mwanya huu kujichotea rasilimali za nchi.

0 Responses to “NEWS ALERT: WAZIRI NYALANDU AMTIMUA PROFESA SONGORWA MBELE YA WABUNGE KIKAONI.”

Post a Comment

More to Read