Saturday, September 17, 2016

SIMBA WAILOWESHA AZAM FC UHURU STADIUM.






Shiza Kichuya amepeleka furaha ya pointi tatu Msimbazi baada ya goli lake kuihakikishia ushindi Simba wakati ikipambana dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru.

Kichuya alipachika bao dakika ya 67 kipindi cha pili na kujifikishia magoli mawili kwenye ligi msimu huu huku bao lake la kwanza akiwa alilifunga kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa taifa.


Simba inafikisha pointi 13 na kuongoza msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 5 ikiwa imeshinda mechi zake 4 na kutoka sare kwenye mchezo mmoja. Kabla ya mchezo wa leo, timu zote (Azam na Simba) zilikuwa zinalingana kwa kila kitu kuanzia pointi, magoli ya kufunga na kufungwa.


Azamwaliokuwa wenyeji wa mchezo dhidi ya Simba, wamepoteza mechi kwa mara ya kwanza baada ya kucheza mechi 5 wakiibuka na ushindi katika mechi 4 na kutoka sare mchezo mmoja na kuendelea kubaki na pointi zao 10 kwenye msimamo wa ligi.

0 Responses to “SIMBA WAILOWESHA AZAM FC UHURU STADIUM.”

Post a Comment

More to Read