Wednesday, May 13, 2015
WAUGUZI HOSPITAL YA RUFAA MBEYA WALIA NA MAGONJWA YA KUSENDEKA
Do you like this story?
Wauguzi wa Hospital ya Rufaa Mbeya wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka huu .Picha EmanuelMadafa jamiimojablog |
Wauguzi wa hospital ya Rufaa Mbeya wakiwasha mishumaa kuungana na wauguzi wengine duninia katika kuadhimisha kilele cha siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka . |
Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya
wakiapa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani. Wakiungana na
Wauguzi wengine Duniani kuadhimishi Siku hii.
|
Wauguzi wa Hospital ya Rufaa Mbeya wakiserebuka katika kuadhimisha kilele cha siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka huu sherehe ambazo zimefanyika katika ukumbi wa Romani Kathoriki jijini Mbeya |
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wauguzi duniani hospital ya Rufaa Mbeya Ndugu Joyce Komba akisoma Lisala kwa mgeni rasmi katika kuadhimisha kilele cha siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka huu . |
Makamu Mwenyekiti wa chama cha wauguzi TANNA Hospital ya Rufaa Mbeya Ndugu Joyce Komba akikabidhi Lisala kwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya wauguzi duninia mei 12 mwaka huu. |
Chama cha wauguzi Tanzania
(TANNA)Hospital ya Rufaa Mbeya wameitaka serikali kuhakikisha inaanzisha
kitengo cha afya ya jamii kwa lengo
utoaji wa tiba kwa wagonjwa wa maambuki ya ugonjwa wa Kusondeka.
Kauli hiyo imetolewa na
Makamu mwenyekiti wa chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) hospitali ya Rufaa
Mbeya Ndugu Joyce Robert katika kilele cha siku ya wauguzi duniani sherehe
ambazo zimefanyika katika ukumbi wa romani kathoriki jijini hapa mei 12 mwaka huu .
Akisoma Lisala kwa mgeni
rasmi makamu huyo mwenyekiti amesema kutokana na kuongezeka kwa magonjwa
kusendeka wauguzi wamekuwa wakipata wakati mgumu namna ya kuwahudumia wagonjwa
wa aina hiyo.
Hivyo amesema kuwa ili
kuondokana na hali hiyo nivema serikali ikajaribu kuona uwezekano wa kuanzisha
kitengo cha afya ya jamii (Public health
department)kitakacho husika moja kwamoja na utoaji huduma kwa wagonjwa wa aina
hiyo badala ya kuachiwa kwa wauguzi
pekee.
Katika hatua nyingine chama
hicho kimeitaka ofisi ofisi ya mkurugenzi wa hospital ya rufaa mbeya
kuhakikisha inafuatilia kwa ukaribu suala la upandishwaji wa vyeo pamoja na ulipwaji
wa malimbikizo yao kwa wakati .
Amesema kwa muda mrefu
wauguzi wamekuwa wakipata adha kubwa kwa ufuatiliaji wa madai yao mara wanapo
koma utumishi wa umma ambapo wengi wao wamekuwa wakifuatilia madai yao wizarani
badala ya ofisi ya mkurugenzi hali ambayo inakatisha taama kwa watumishi hao.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAUGUZI HOSPITAL YA RUFAA MBEYA WALIA NA MAGONJWA YA KUSENDEKA”
Post a Comment