Wednesday, April 15, 2015
WAZEE WASTAAFU WALALAMIKIA MALIPO YA PENSHENI ZAO.
Do you like this story?
Wazee
wastaafu wanaochukua pensheni zao kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF
wameulalamikia mfuko huo kwa kutowalipa fedha zao mpaka sasa.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo mjini
hapa wazee hao wamesema kuwa kwa kawaida walitakiwa kupokea pensheni zao tangu
April mosi mwaka huu lakini mpaka sasa hawajalipwa bila ya kuelezwa sababu
zozote za msingi.
Akizungumza kwa niaba ya wazee hao, Ndijina
Ndilito alisema kuwa tangu April mosi mwaka huu wamekuwa wakienda benki
kuangalia kama fedha zao za pensheni lakini mpaka jana zilikuwa hazijaingia.
Alisema walipokwenda kwenye ofisi za PSPF
mkoa wa Dodoma kuulizia kwa nini fedha zao hazijaingia mpaka muda huu
waliambiwa kuwa fedha zao zimtumwa makao makuu ya benki ya NMB ambako
wanachukulia fedha zao hivyo waendelee kusubiria mpaka hapo zitakapoingia.
Kwa upande wake ofisa wa PSPF Mkoa wa Dodoma,
Rahim Hashim amesema kuwa yeye siyo msemaji wa mfuko huo na kwamba msemaji mkuu
wa mfuko huo ni Mkurugenzi mkuu wa PSPF.
Hata hivyo Mkurugenzi mkuu wa PSPF Adamu
Mayingu alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo simu yake ya mkononi iliita bila
kupokelewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZEE WASTAAFU WALALAMIKIA MALIPO YA PENSHENI ZAO.”
Post a Comment