Wednesday, April 15, 2015

SERIKALI KUVIFUTA VYAMA VITAKAVYO KIUKA SHERIA.


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mathiaus Chikawe.


Serikali ya Tanzania imesema kuwa kuanzia tarehe 20 mwezi huu itaanza kuvifuta vyama vyote vyote vilivyosajiliwa chini ya sheria ya vyama sura namba 337 ambavyo havitafuata matakwa ya kisheria.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akitoka mustakabali wa nchi kuelekea zoezi la kura ya maoni kuhusu katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu ujayo.

Katika hatua nyinghine Mh. Chikawe amevitaka vyama vya siasa kuepuka siasa za uchochezi na uvunjifu wa amani ikiwemo kuacha ushabiki wa kuwatoa wanachama sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa kufanya hivyo kutapunguza uhasama ulioanza kujitokeza siku za karibuni.
Aidha Mh Chikawe amewataka viongozi wa dini kuacha kuingilia masuala ya kisiasa na kwani ni kinyume cha sheria ya vyama pamoja na katiba zinazosimamia uendeshaji wa taasisi zao.

Chikawe amesema viongozi wana haki ya kushiriki masuala ya kisiasa kama watu binafsi lakini si kuwashawishi waumini wao watekeleze matakwa yao ya kisiasa kwa manufaa yao.

0 Responses to “SERIKALI KUVIFUTA VYAMA VITAKAVYO KIUKA SHERIA.”

Post a Comment

More to Read