Wednesday, May 13, 2015

BOW WOW AJITOA CASH MONEY.




New York, Marekani
RAPA aliyeanza muziki tangu akiwa na miaka mitano, Bow Wow, amejitoa kwenye Lebo ya Cash Money ambayo alidumu nayo kwa miaka mitano sasa.

Bow Wow aliyetesa na Kibao cha Let Me Hold You, ameamua kujitoa kwenye lebo hiyo aliyosaini miaka mitano iliyopita kutokana na kutopata mafanikio yoyote ya kimuziki mpaka sasa.

Alitumia muda wake kuposti video kwenye Mtandao wa Facebook akisema anaondoka kwa amani na kuongeza kuwa hana tatizo na Cash Money wala Birdman.
Tangu ajiunge kwenye lebo hiyo, Bow Wow hakufanikiwa kuachia albamu yoyote ya peke yake licha ya kurekodi ngoma kibao alizoishia kuzisikiliza yeye tu, kitu ambacho kilimuuma zaidi.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa nyota huyo anarejea kufanya kazi chini ya mastaa waliogundua kipaji chake tangu akiwa mtoto, Snoop Dogg na Jermaine Dupri na hivi karibuni ataachia singo yake mpya.

0 Responses to “BOW WOW AJITOA CASH MONEY.”

Post a Comment

More to Read