Wednesday, May 13, 2015
KIM JONG-UN AMUUA WAZIRI WA ULINZI KWA KUSINZIA KWENYE MKUTANO WAKE
Do you like this story?
Hyon Yong-Chol aliyeuawa kwa kusinzia wakati wa hafla ya kijeshi. |
WAZIRI
wa Ulinzi wa Korea ya Kaskazini, Hyon Yong-Chol, ameuawa kwa kupigwa na bunduki
ya kutungulia ndege aina ya ZPU-4 kwa kusinzia kwenye hafla ya kijeshi. Waziri
huyo aliuawa kutokana na amri ya kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-Un.
Sababu nyingine iliyomfanya waziri huyo
aliyekuwa na umri wa miaka 66 na aliyekuwa kiongozi wa jeshi la nchi hiyo tangu
mwaka 2012 auawe, ni kutoa kauli za kumpinga kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-Un
katika matukio kadhaa.
Hyon aliuawa mbele ya mamia ya maofisa wa
serikali na jeshi katika kambi moja mjini Pyongyang tarehe 30 Aprili mwaka huu
ambapo aliyemuua alisimama umbali wa futi 100 tu akitumia bunduki hiyo ambayo
inaweza kufika umbali wa futi 26,000.
Uchunguzi
umeonyesha kwamba watu wengi waliuawa kwa kutumia njia hiyo ya kikatili katika
kambi hiyo mwezi Oktoba mwaka jana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIM JONG-UN AMUUA WAZIRI WA ULINZI KWA KUSINZIA KWENYE MKUTANO WAKE”
Post a Comment