Monday, September 26, 2016

YANGA WAAMUA KUWAENDEA SIMBA PEMBA




MSAFARA wa kikosi cha Yanga SC umeondoka Mwanza asubuhi ya leo kuelekea Pemba kwa ajili ya kambi ya wiki 1, Yanga waliwasili Mwanza alfajiri ya leo wakitokea Shinyanga kisha kuunganisha kwenda kisiwani pemba kwa usafiri wa Ndege.

Yanga wameondoka huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa VPL jana dhidi ya Wapiga Debe wa Standa United ya Shinyanga baada ya kufungwa bao 1-0.

Wakali hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani wameekea mjini Pemba kuweka kambi maalum kwaajili ya kuwavaa mahasimu wao Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Oktoba Mosi jijini Dar es Salaam.

0 Responses to “YANGA WAAMUA KUWAENDEA SIMBA PEMBA”

Post a Comment

More to Read