Wednesday, May 13, 2015

BARCELONA YATINGA NUSU FAINALI.





WAZEE wa soka la burudani, FC Barcelona wametinga fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-3 dhidi ya FC Bayern Munich ya Pep Guardiola.

Mechi ya kwanza Camp Nou, Barcelona walishinda 3-0 na jana usiku wakali hayo wa 'Katalunya' wamekufa 3-2 dimba la Allianz Arena mjini Munich.

Magoli ya Bayern yalifungwa na Mehdi Benatia dakika ya 7', Roberto Lewandowski 59' na Thomas Muller dakika ya 74, wakati nyota wa Brazil, Neymar Jr alifunga magoli yote mawili ya Barcelona dakika za 15' na 29' akipokea pazi zote kutoka kwa Luis Suarez.

Ukiachana na matokeo, soka lilikuwa zuri, Bayern walijitahidi kupambana na kumiliki mpira kwa asilimia 54 dhidi ya 46, lakini Barcelona si timu ya kuisogelea kirahisi.
Bayern walifika langoni kwa Barca na kupiga mashuti 8 yaliyolenga lango wakati wageni wao walipiga matano (5) tu.

Kitu cha kushangaza, Barca hawakupiga shuti lolote ambalo halikulenga lango, lakini Bayern waliokuwa na papara walipiga mashuti 10 yasiyolenga lango.

0 Responses to “BARCELONA YATINGA NUSU FAINALI.”

Post a Comment

More to Read