Saturday, May 3, 2014
MKUU WA WILAYA ATISHIWA BAADA YA KUVUNJA DANGURO, MKUU WA MKOA AZUNGUMZIA SAKATA HILO.
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Meck Sadik amekanusha tuhuma zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku
(si HabariLeo) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema
ametishiwa maisha baada ya kuvunja danguro la Temeke.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mkuu
huyo wa Mkoa alisema gazeti hilo liliandika habari hiyo ambayo si ya kweli na
kuongeza kuwa ina lengo la kudidimiza operesheni hiyo.
“Naomba niwatoe hofu habari hizo si za
kweli na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema ametueleza kuwa si kweli na hivyo
tunaamini mwandishi wa habari hiyo hana lengo zuri,” alisema Sadik.
Aliongeza kuwa danguro hilo lilikuwa ni
kichaka cha wanawake wadogo wanaojihusisha na ngono, wavuta bangi na dawa
za kulevya.
“Kwa kweli kama kuna madanguro mengine
tunaomba yafichuliwe ili wanaofanya biashara hizo waweze kuchukuliwa hatua za
kisheria haraka na tunaahidi kuwa operesheni hii itakuwa endelevu,” amesema.
Aidha alitoa rai kwa wananchi ambao
katika mitaa wanayoishi kuna madanguro watoe taarifa hizo haraka kwa vyombo vya
usalama ili hatua zichukuliwe mara moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MKUU WA WILAYA ATISHIWA BAADA YA KUVUNJA DANGURO, MKUU WA MKOA AZUNGUMZIA SAKATA HILO.”
Post a Comment