Sunday, April 27, 2014
VURUGU ZAFUMUKA KAMBI YA UJENZI SUMBAWANGA.
Do you like this story?
Polisi mjini hapa wamelazimika kutumia
risasi za moto kutawanya wafanyakazi wa Kampuni ya Aaarsleef /Bam
International inayojenga kwa kiwango cha lami kipande cha
barabara cha Laela - Sumbawanga waliofunga barabara eneo la Kianda.
Wafanyakazi hao walifunga barabara wakipinga kitendo cha walinzi wa kampuni hiyo kumzuia mwenzao mmoja wakimtuhumu kutaka kuiba mafuta.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa mkasa huo wafanyakazi hao wa kambi ya ujenzi ya Kianda wilayani Sumbawanga walileta usumbufu mkubwa wakipinga walinzi wa kampuni hiyo kumkamata opereta wa tingatinga, aitwaye Gabriel Daniel (34) mkazi wa eneo la Bomani , Manispaa ya Sumbawanga.
Kufuatia dhahama hiyo wafanyakazi hao wenye hasira waliteketeza kwa moto magari makubwa manne. Magari hayo ni pamoja na Scania Tipper lenye namba za usajili T 755 CAV, Iveco lenye namba za usajili T 116 AYT , gari aina ya Artego lenye nambari za usajili T 839 na gari aina ya Artois yenye namba za usajili T 936.
Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.
Watuhumiwa hao ni Emanuel Sanga
(34) mkazi wa Mkoa wa Iringa na Ngasa Mathias (40)
mkazi wa wilayani Chunya, Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ VURUGU ZAFUMUKA KAMBI YA UJENZI SUMBAWANGA.”
Post a Comment