Sunday, April 27, 2014
DANSA WA DIAMOND AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA, WACHINA WAAMUA KUSAKA DIAMOND.
Do you like this story?
STAA wa muziki wa bongo fleva nchini, Abdul Nassib "Diamond" ametakiwa kutokanyaga kabisa nchini China na kwamba akitokeza pua yake nchini humo asahau kabisa kurudi uraiani...
Hiyo inafuatia kijana
mmoja mtanzania kukamatwa wiki iliyopita
uwanja wa ndege wa Macau China
na kudai kuwa yeye ni mcheza shoo
wa mwanamuziki Diamond kutoka Tanzania....
Habari kutoka Macau
China zinadai kuwa kijana huyo
aliyejulikana kwa jina moja la Manyota
alikamatwa akiwa kwenye harakati za
kuingiza mzigo huo wa dawa za kulevya
kwa kupitia uwanja wa ndege wa Macau....
Kwa mujibu wa
vyanzo vyetu vya habari, inaarifiwa kuwa
Manyota alikamatwa Alhamisi ya wiki
iliyopita katika uwanja uleule aliokamatwa
mtanzania mwingine Jackline Patrick, anayesotea
rumande mpaka hii leo huko huko Macau
China.....
Kijana mmoja wa
kitanzania anayefanya shughuli zake huko
China amedai kuwa Manyota alikamatwa na
maofisa wa usalama wa uwanja wa ndege
na katika utetezi wake alidai kuwa
yeye ni mwanamuziki toka Afrika Mashariki...
Mtanzania huyo
aliendelea kudai kuwa, Manyota baada ya
kukamatwa alianza kubabaika kwa kujifanya
mwanamuziki na baadae akadai kuwa yeye
ni mcheza shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka
Tanzania....
"Alijifanya yeye
ni mwanamuziki, baadae akabadilika na kudai
yeye ni mcheza shoo wa mwanamuziki
Diamond kutoka Tanzania na kwamba ndani
ya ule mzigo alikuwa hajui kuna nini
zaidi ya kuombwa na jamaa zake wa
Dar awapelekee nchini China"...Alisema
mtanzania huyo
Inasemekana kuwa, ili
kujiridhisha, maofisa hao wa usalama wa uwanja
wa ndege walimtaka kijana huyo
aoneshe moja ya kazi zake na yeye
akaishia kuwaonesha moja ya video za
Diamond kupitia mtandaoni na kumuonesha
mmoja wa wacheza shoo wa mwanamuziki
huyo kuwa ndo yeye Manyota...
Inasemekana kuwa, pamoja
na utetezi wake huo ambao unaweza
kumuingiza matatani Diamond,maofisa hao wa
usalama walishndwa kumuelewa na kumtupa
ndani.....
Mtanzania huyo
alihitimisha kwa kudai kuwa, kutokana na
mazingira yalivyo,ni vyema mwanamuzi Diamond
akawa makini sana kama atakuwa na safari
za kwenda China kwani kwa namna moja
ama nyingine jina lake limewekwa kwenye
orodha ya majina machafu na wanaweza
kumkamata kwa lengo la kuujua ukweli....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DANSA WA DIAMOND AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA, WACHINA WAAMUA KUSAKA DIAMOND.”
Post a Comment