Tuesday, April 22, 2014

HUU NI UKATILI NA UNYANYASAJI TAZAMA PICHA MTOTO AFUNGWA KAMBA ASITOKE NYUMBANI KWAO.


Mtoto Samir mkazi wa mtaa wa Langoni kata ya Miembeni,akiwa amefungwa kamba katika mguu wake wa kushoto huku upande mwingine ukiwa umefungwa katika chuma kizito kilichopo jirani na mlango.



Na Dixon Busagaga
MTOTO Samir anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano mkazi wa mtaa wa Langoni katika manispaa ya Moshi, amejikuta katika wakati mgumu kutokana na tabia ya bibi yake kumfunga kamba katika mguu wake kwa lengo la kumzuia asiende kucheza mbali na nyumbani kwao.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika eneo hilo ambapo bibi huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alikutwa akiwa amemfunga kamba ya kudu mjukuu wake huyo katika mguu wa kushoto huku sehemu nyingine ikiwa imefungwa katika chuma kizito. 

Kwa mujibu wa majirani walisema bibi huyo amekuwa akimfunga mtoto huyo mara kwa mara kwa zaidi ya nusu saa hasa nyakati ambazo bibi huyo amekuwa akifanya shughuli zake za usafi wa ndani pamoja na kufua.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina,majirani hao wamesema imekuwa ni kawaida kwa bibi huyo ambaye anaishi na wajukuu zake kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo huku akimzuia kucheza na wenzake wa nyumba za jirani.

“Sisi hiyo hali mbona tumeizoea mara kwa mara Samir akienda kucheza na wenzake huko mtaani,bibi yake akimkuta huko anamkamata na kisha kumfunga kwenye hilo chuma lililoko hapo mlangoni kwa zaidi hata ya nusu saa”alisema mmoja wa majirani.

0 Responses to “HUU NI UKATILI NA UNYANYASAJI TAZAMA PICHA MTOTO AFUNGWA KAMBA ASITOKE NYUMBANI KWAO.”

Post a Comment

More to Read