Friday, April 4, 2014
UGONJWA WA HATARI WAUA WATU 10 DAR, WENGINE 70 WAUGUA.
Do you like this story?
Ugonjwa wa homa ya dengue ulioibuka jijini Dar es Salaam kuanzia mwishoni
mwa Januari, mwaka huu umeathiri watu 10 na mmoja amefariki dunia. Mganga
Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando alisema hayo hivi karibuni alipozungumza na
mwandishi na kusema baada ya kupungua kwa ugonjwa wa malaria, umeibuka
ugonjwa huo.
Alisema tangu uthibitishwe kuwepo nchini Januari mwaka huu, hadi
sasa idadi ya watu ambao wamethibishwa kuugua ugonjwa huo ni 70.
Kwa mujibu wa Dk Mmbando, katika wiki mbili zilizopita,
idadi ya wagonjwa imeongezeka mara mbili kuliko siku za nyuma. Alisema
kifo kilichotokana na ugonjwa huo, kilitokea katika Hospitali ya Mwananyamala.
Alisema ugonjwa wa malaria umepungua kutoka asilimia 80 hadi chini ya 10
kutokana na kuwa juhudi zilielekezwa zaidi katika kudhibiti ugonjwa wa malaria
pekee bila kujali wanaoambukiza magonjwa mengine.
“Mpango wa serikali sasa ni kudhibiti mbu wote wanaouma mchana na usiku bila
kujali wanaambukiza magonjwa gani ili kuweza kupambana na homa hii inayoibuka
kwa kasi,” alisema.
Dk Mmbando alisema sasa wanaandaa taarifa muhimu na mikakati ya kudhibiti
ugonjwa huo na kutoa taarifa kwa wananchi.
Katika taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Seif Suleiman Rashidi ilisema ugonjwa huo si mpya nchini,
kwani uligundulika kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es
Salaam, ambapo idadi ya watu waliothibitika kuwa na ugonjwa ilikuwa 40.
Alisema pia kati ya Mei na Julai 2013, wagonjwa 172 walithibitishwa
kuwa na ugonjwa huu na hakuna aliyepoteza maisha.
Waziri alishauri jamii kutokuwa na hofu kuhusu ugonjwa huo,
isipokuwa waende kwenye vituo vya tiba wanapoona dalili.
Alishauri wahakikishe mazalio yote ya mbu yanaangamizwa na pia kuzuia
kuumwa na mbu.
Alisema hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili ya wasafiri
wanaoingia na wanaotoka nchini. Alisema wizara itaendelea kushirikiana na sekta
mbalimbali, kufuatilia na kudhibiti ugonjwa huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UGONJWA WA HATARI WAUA WATU 10 DAR, WENGINE 70 WAUGUA.”
Post a Comment