Friday, April 4, 2014
LUGOLA; KUKUBALI SERIKALI TATU NI KUKWEPA UNAFIKI.
Do you like this story?
Mjumbe wa Bunge la Katiba Kangi Lugola,
ametaja msimamo wake wa kuunga mkono serikali tatu kwamba ni kukwepa unafiki.
Lugola, ambaye alisema kwenye kikao cha Bunge
la Katiba kuwa atakuwa wa mwisho kuisaliti Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
alisema kinachowasumbua wanasiasa wengi ni suala la unafiki ambalo ameapa
hatakuwa tayari kulisujudia.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu msimamo
wake unaopingana na chama chake cha CCM, alisema wanaounga mkono miongozo ya
vyama kwenye Bunge la Katiba, wanafanya hivyo kwa unafiki na hofu ya kisiasa.
Alisema kitendo cha kupinga Rasimu ya
Pili ya Katiba ambayo iliwasilishwa na mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph
Warioba, ni sawa na kupinga mawazo ya wananchi.
“Tumetumia fedha nyingi kwa ajili ya Tume ya Jaji
Warioba kukusanya maoni ya wananchi na alichokileta bungeni ni matakwa ya
Watanzania. Leo hii tunaanza kuchakachua kile ambacho alikifanyia kazi kwa
uaminifu mkubwa?” alihoji Lugola.
Alisema hawezi kukubaliana na dhambi ya
unafiki. “Nawataka wana-CCM wenzangu muweze kupima mambo badala ya kuburutwa,”
alisema.
Kuhusu muundo wa Muungano, alisema hata sasa
hakuna Muungano kwani Zanzibar imeshajitangazia mamlaka yake.
“Kama wanataka kurudisha Muungano, Serikali
ya Zanzibar inatakiwa ivunjwe ili ieleweke kuwa hakuna Tanganyika na hakuna
Zanzibar. Sasa hakuna lolote ambalo linaweza kunishawishi kuwa kuna Muungano,”
alisema Lugola.
“Muundo wa be huyo alisema kuwa serikali tatu
unawezekana na tayari upo unafanya kazi, lakini ukiwa katika kivuli cha Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,” alisema ambaye wiki iliyopita aliwatahadharisha
wajumbe wenzake dhidi ya hatari kwa wengi kuwaburuza wachache.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LUGOLA; KUKUBALI SERIKALI TATU NI KUKWEPA UNAFIKI.”
Post a Comment