Tuesday, May 6, 2014

BUNGE LA BAJETI LAANZA LEO, HIZI NI POSHO MPYA WALIZOONGEZEWA WABUNGE.


Baada ya kuhairishwa kwa Bunge la maalum la Katiba,Bunge la bajeti linaanza leo Mei 06 Dodoma ambapo wabunge wanatarajiwa kuanza kulipwa viwango vipya vya posho ambapo itakua ni shilingi 300,000 kwa siku ambayo ni sawa na viwango sawa na walivyokuwa wakilipwa wajumbe bunge maalum la katiba.

Kabla ya kupandishwa kwa posho hizo Wabunge walikua wakilipwa 200,000 kwa siku ambayo mgawanyo wake ulikua ni sawa na 70,000 kama posho ya kikao,80,000 posho ya kujikimu na 50,000 gharama za usafiri...

Nyongeza hiyo ya kila mbunge ambayo ni nyongeza sawa na asimilia 50 litaigharimu Bunge la Jamhuri ya Muungano kiasi cha Tsh Bilioni 18.5 kwa siku 52 zilizotengwa kwa ajili ya bunge hilo la bajeti.
 
Bunge hili linategemea kumalizika June 27.

0 Responses to “BUNGE LA BAJETI LAANZA LEO, HIZI NI POSHO MPYA WALIZOONGEZEWA WABUNGE.”

Post a Comment

More to Read