Thursday, May 1, 2014
HII NDIO NCHI ILIYOPITISHA SHERIA YA WEZI KUKATWA MIKONO NA WAZINIFU KUPIGWA MAWE HADI KUFA.
Do you like this story?
Sultani na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani. |
Serikali ya
Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za
kiisilamu.
Kiongozi wa
nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo
itaanza kutumika kuanzia wiki hii.
Adhabu zilizo
chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe
hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa.
Sheria hii
itatekelzwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa
Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.
Taifa la
Brunei tayari linafuata sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama
Malaysia na Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe.
Nchi hiyo
ndogo ilio katika kisiwa cha Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah na
imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje mafuta na gesi yake.
Takriban nusu
ya waisilamu wanaoishi katika nchi hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani
alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo
akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa
sheria hiyo.
Sheria
yenyewe itaanza kutumika katika kipindi cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa
ya kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa faini.
Katika awamu
ya pili ndipo wahalifu wataanza kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia ya
wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi
ya jinsia moja.
Sultani
anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani na tayari
amewaonya watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia mitandao ya kijamii.
Mfumo wa
sheria katika mahakama nchini humo ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja wa
Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria
hiyo inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HII NDIO NCHI ILIYOPITISHA SHERIA YA WEZI KUKATWA MIKONO NA WAZINIFU KUPIGWA MAWE HADI KUFA.”
Post a Comment