Tuesday, May 20, 2014
JK KUONGOZA MASHAURIANO YA MRADI WA MABASI.
Do you like this story?
Dar es
Salaam. Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuongoza mkutano wa mashauriano ya awamu
ya kwanza ya uwekezaji katika mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART)
utakaowakutanisha wawekezaji wa ndani na nje Dar es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa DART, Asteria Mlambo alisema mwishoni mwa wiki kuwa mkutano huo
utakaofanyika mapema mwezi ujao utatoa nafasi kwa wawekezaji kuzijua fursa za
uwekezaji zitakazopatika kwenye mradi huo.
Washiriki
wa mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika benki na taasisi mbalimbali za
kifedha, kampuni za kutengeneza mabasi, kampuni za mawasiliano, mifuko ya
kijamii na wengine.
Mada
kuhusu mradi wenyewe wa DART itatolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Tamisemi), Jumanne Sagini.
Kabla
ya mkutano huo, DART imeandaa mkutano wa wamiliki wa daladala Dar es Salaam,
Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na wadau wengine ili kuwafahamisha
jinsi gani wanaweza kunufaika na mfumo huo mpya.
“Tutawaelezea
faida na fursa zitakazopatikana kwenye mfumo mpya wa usafirishaji jijini,”
alisema Mlambo.
Mwezi
uliopita Dart ilikamilisha shughuli ya kusajili mabasi ya daladala yanayopita
katika Barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo ikiwa ni moja ya
matayarisho ya kupisha mradi huo.
Kulingana
na mpango huo wa Dart barabara hizo za Morogoro, Kawawa na Msimbazi zitatumiwa
na mabasi ya mfumo huo pekee kwa njia 64 Dar es Salaam zitakoma kutumika
kutokana na mradi huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JK KUONGOZA MASHAURIANO YA MRADI WA MABASI.”
Post a Comment