Monday, May 19, 2014
MBATIA KUTOA MILIONI 10 KWA PROFESA ATAKAYEPATA MASWALI YOTE YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MWAKA JANA
Do you like this story?
Changamoto ya
mapungufu yaliyotajwa kwenye maandalizi ya vitabu na mitihani ya kumaliza
darasa la saba imepelekea mheshimiwa James Mbatia kuwa-challenge maprofesa
walioko bungeni kuufanya mtihani wa darasa la saba ambao kwa mujibu wake
haufanyiki.
Akitoa
mchango wake bungeni wakati wa mjadala kuhusu bajeti ya wizara ya elimu na
mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, Mbatia amesema alichukua mtihani wa
darasa la saba na kuupeleka kwa professor wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na
alimrudishia majibu kuwa mtihani ule haufanyiki.
“Njoo kwenye
mtihani wa hisabati, na mimi napenda sana hisabati. Mheshimiwa spika,
nilipeleka mtihani huu kwa professor wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, mtihani
wa darasa la saba. Professor ameniandikia hapa ‘nimetumia muda wa saa
mbili na dakika tatu kufanya mtihani huu bila kuandika majibu kwenye karatasi
na mtihani wenyewe haufanyiki.
"Yaani
ni madudu matupu yako kwenye mtihani huu. Nawachallenge wenzangu ambao ni
maprofesa na wengine wanajua hisabati, wafanye mtihani huu waweze kupata
100/100 na mimi ntawapa shilingi milioni 10 ndani ya bunge hili.” Amesema James Mbatia.
Mbatia
aliendelea kuweka msisitizo kuwa angeweza kuuweka mtihani huo kwenye meza
bungeni hapo na professor yeyete ambaye ataweza kuufanya na kupata 100/100
angempa shilingi milioni 10.
Ameukosoa
vikali mpango wa ‘matokeo makubwa sasa’ ambao amedai utekelezaji wake umegeuka
kuwa madudu yanayotisha kwenye elimu ya Tanzania.
“Mheshimiwa
naibu spika haya ni mambo ya kusikitisha, ni mambo ya kutisha. Na nchi yetu
elimu ni dhaifu ya kupindukia. Elimu ni mapigo wa moyo ya taifa. Mapigo ya moyo
yakienda kinyume na utaratibu wake maisha hupotea. Kwa hiyo uhai wa taifa la
Tanzania hupotea kwa sababu tumeshindwa kuwekeza kwenye elimu. Wanafunzi wetu
wanashindwa kufikiri yakinifu. Power of reasoning katika nchi yetu imekwenda
chini sana kwa sababu elimu yetu ni dhaifu, ni dhaifu ya kutisha.” Ameongeza.
Amependekeza
kuwa ili kupata tiba, bunge limuombe rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya kudumu
ya elimu nchini ambayo itakayokuwa inahakikisha ubora wa elimu na kudhibiti
mambo yanayosababisha kutetereka kwa elimu nchini na amependekeza iitwe
‘Education quality assurance and control’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBATIA KUTOA MILIONI 10 KWA PROFESA ATAKAYEPATA MASWALI YOTE YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MWAKA JANA”
Post a Comment