Monday, May 19, 2014
MUUGUZI MWENYE VVU AFUNGWA JELA MIAKA 3 BAADA YA KUMCHOMA SINDANO MTOTO NA KUMUAMBUKIZA VIRUSI
Do you like this story?
Nchini Uganda mahakama imempata na
hatia muuguzi mwenye HIV, aliyeshitakiwa kwa kumdunga mtoto mchanga sindano,
ambayo awali ilimchoma yeye mwenyewe.
Muunguzi huyo, Rosemary Namubiru,
mwenye umri wa miaka 64, mwathiriwa wa virusi vya HIV, amefungwa miaka mitatu
jela, kwa kile hakimu amekiita, 'uzembe wa weledi'.
Hukumu hio imetolewa wiki moja baada ya
bunge la Uganda kupitisha muswada, unaomtia hatiani mtu yeyote ambaye kusudi
anamuambukiza mtu mwengine virusi vya ukimwi.
Mtoto huyo hata hivyo hakuambukizwa
virusi vya HIV na wanaharakati wamekosoa mahakama kwa kumfunga jela mwanamke
huyo.
Babake mtoto huyo hata hivyo alielezea
kufurahishwa na uamuzi wa mahakama.
Baba huyo, Daniel Mushabe, amesema kuwa
anatumai kesi hiyo itampa motisha Rais Museveni kuidhinisha mswada uliopitishwa
na wabunge wa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaowaambukiza wengine HIV
kusudi.
Adhabu ya kosa hilo ni faini ya dola
1,900 au miaka kumi jela.
Sheria hiyo ikiwa itapitishwa
itawaadhibu wanaotenda uhalifu huo kwa maksudi.
Wananchi bila shaka walionyesha
kuudhiwa na kitendo cha muuguzi huyo ingawa wanaharakati wamemtetea mama
muuguzi.
Hakimu aliyetoa hukumu alisema kuwa
Namubiru alikosa kuonekana kama aiyesikitishwa na kosa lake.
Namubiru, muuguzi mwenye uzoefu wa kazi
wa miaka 30, alisisitiza kwamba hana hatia na kuwa mtoto huyo hakuambukizwa
HIV.
Namubiru aliamua kumdunga sindano mtoto
huyo kutafuta mshipa lakini kapata ugumu na hivyo kujidunga mwenye kwa bahati
mbaya lakini amesisitiza kuwa hakuwa na nia yoyote ya kumuambukiza mtoto huyo
virusi vya HIV.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MUUGUZI MWENYE VVU AFUNGWA JELA MIAKA 3 BAADA YA KUMCHOMA SINDANO MTOTO NA KUMUAMBUKIZA VIRUSI”
Post a Comment