Tuesday, May 20, 2014
WANAFUNZI WAPINGA KUONGEZA KARO KENYA.
Do you like this story?
Wanafunzi
wa vyuo vikuu nchini Kenya wamezua vurugu wakipinga mpango wa serikali kutaka
kuongeza karo katika vyuo vikuu vyote vya umma.
Polisi
walipambana na wanafunzi hao kwa kutumia gesi ya kutoa machozi kutawanya
wanafunzi hao ambao walizua vurugu mjini na kuwapora abiria huku wakiharibu
magari ya umma na yale ya abiria katika barabara kuu ya Uhuru katikakati ya
jiji la Nairobi.
Pia
waliripotiwa kuvunja maduka na kuharibu mali ya watu.
Wachuuzi
walilazimika kuondoka mjini huku polisi wakipambana na wanafunzi hao ambao
waliungana kutoka vyuo vikuu mbali mbali kote nchini Kenya.
Awali
maandamano yao yalikuwa salama ingawa baadaye wanafunzi hao walioanza
kuandamana tangu saa nne asubuhi walianza kuzua rabsha na kulazimisha polisi
kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.
Wanafunzi
hao wanaandamana kupinga mapendekezo ya serikali kuongeza karo ya vyo vikuu ,
ingawa waziri wa elimu ya juu Profesa Jacob Kaimenyi amesema kuwa serikali bado
haijatoa tamko rasmi ikiwa wanafunzi wa vyuo vikuu watalazimika kuongeza karo.
Alisema
kuwa ripoti kuwa karo itaongezwa sio sawa na ni za kupotosha akisisitiza kuwa
ikiwa jambo kama hilo litafanyika litahitajika kutangazwa na baraza la vyuo
vikuu nchini humo baada ya makubaliano kufikiwa.
Wanafunzi
hao wanapinga mpango wa serikali wakisema kuwa kuambatana na mfumuko wa bei,
karo yao haipaswi kuongezwa na kwamba serikali inapaswa kushauriana nao kabla
ya kufikia hatua zozote za kuongeza karo.
Wanafunzi
watano wameripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI WAPINGA KUONGEZA KARO KENYA.”
Post a Comment