Monday, June 30, 2014
DK SALIM AFICHUA SIRI YA JK NA TUME YA WARIOBA.
Do you like this story?
Waziri
Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema hakutarajia kusikia kauli za Rais
Jakaya Kikwete alizozitoa bungeni kukosoa Rasimu Tume ya Mabadiliko ya Katiba
kwa sababu walikuwa wanampa taarifa kwa kila hatua waliyokuwa wanafikia kabla
ya kutoa rasimu hiyo.
Dk
Salim alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake
Masaki, Dar es Salaam wiki iliyopita.
“Hatukutarajia
kama hali ingefikia hatua iliyofikia,” alisema Dk Salim na kuongeza: “Lakini
Rais ana uamuzi wake na anazingatia mambo mengine mengi.”
Akilihutubia
Bunge maalumu la Katiba Machi 21, mwaka huu Rais Kikwete aligusia mambo saba ya
msingi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na kutaka yatazamwe kwa kina, huku
akibainisha kuwa mengine hayawezekani kutekelezeka. Miongoni mwa mambo hayo ni
muundo wa Serikali. Alipinga waziwazi pendekezo la serikali tatu
lililopendekezwa na Tume na kuegemea katika muundo wa serikali mbili na idadi
ya watu walioupendekeza akionyesha kuwa ilikuwa ni ndogo.
Pia
alisema ni vigumu kutenganisha uwaziri na ubunge kama ilivyokuwa imependekezwa
na Tume kwa maelezo kuwa mawaziri wanatakiwa kuwepo bungeni ili kujibu hoja za
Serikali.
Jambo
lingine alilokosoa katika Rasimu ni pendekezo la mtu kupoteza ubunge kwa sababu
ya kuugua kwa miezi sita mfululizo huku akisema baadhi ya vifungu vya Katiba
vinayopendekezwa vimekuwa na mambo mengi ambayo hayapaswi kuwamo katika Katiba,
bali katika sheria zinazotafsiri utekelezaji wa Katiba yenyewe.
Katika
mahojiano hayo maalumu, Dk Salim alisema baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume
aliacha kuhudhuria vikao vya chama chake ili aweze kufanya kazi hiyo kwa
usahihi na alimtaarifu Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais na katibu mkuu wake na
walimwelewa.
Alipoulizwa
anaitazama vipi Tanzania iwapo Katiba Mpya haitapatikana, Dk Salim alisema ana
wasiwasi kwa kuwa suala hilo limeingizwa siasa na Bunge Maalumu limegeuka la
kisiasa hivyo linaweza kuleta matatizo.
“Tuko
katika hali ambayo si nzuri inayohitaji uongozi thabiti, viongozi wote watambue
umuhimu wa zoezi hili kwa lengo la kulinda amani na utulivu wa nchi yetu,”
alisema.
Alisema
kunahitajika ufumbuzi wa kudumu na hicho ndicho kipimo cha uongozi kwa CCM,
Chadema na wengine kwa kutafakari masilahi ya Watanzania wa leo, kesho na
keshokutwa.
Dk
Salim alisema jambo muhimu sasa ni pande mbili zinazoshindana kuhusu idadi ya
Serikali kutumia mwezi ujao wa Julai kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao ili
Bunge la Katiba liendelee bila misuguano.
Via>Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DK SALIM AFICHUA SIRI YA JK NA TUME YA WARIOBA.”
Post a Comment