Monday, June 30, 2014

TANZANIA PRISONS YAACHA WACHEZAJI WANNE.



Timu ya Tanzania Prisons ya jijini hapa imewafungashia virago wachezaji wake wanane kati ya 11 waliomaliza mikataba ya kuichezea timu hiyo kwa msimu uliopita.

Meneja mpya wa timu hiyo, Enock Mwanguku, alisema kuwa wachezaji 11 wamemaliza mikataba yao, lakini wachezaji wanane lazima waondoke huku watatu akisema upo uwezekano wa kuendelea nao.

“Ni kweli kuna wachezaji 11 walioitumikia Tanzania Prisons msimu uliopita mikataba yao imekwisha, ila siwezi kukupa majina yao ingawa wachezaji watatu kati yao wataendelea kuitumikia timu yetu,” alisema Mwanguku.

Hata hivyo, habari za uhakika zilizopatikana ziliwataja baadhi ya wachezaji ambao wameonyeshwa mlango wa kutokea kuwa ni Brighton Mponzi, Mweta Abdul, na Sixtus  Mwasekaga, ambaye tayari ameshasajiliwa na timu ya Polisi Morogoro.

0 Responses to “TANZANIA PRISONS YAACHA WACHEZAJI WANNE.”

Post a Comment

More to Read