Wednesday, December 2, 2015
SHULE YA MSINGI AZIMIO YA BOMOLEWA KUPISHA UJENZI MPYA WA JENGO LA KISASA MBEYA
Do you like this story?
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Dk Samuel Lazaro akiongea na waandishi wa Habari |
Mwenekano wa Shule ya Msingi Azimio amabayo inatakiwa kubomolewa na kujengwa upya(Picha na Kenneth Ngelesi |
NA
MWANDISHI WETU,MBEYA
BAADHI
ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Azimio Jijini hapa,
wameutaka uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, kuwatafutia watoto wao
shule nyingine kwa ajili ya kuendelea na masomo wakati ujenzi mpya ukiendelea.
Wazazi
hao walisema, halmashauri hiyo inapaswa kuchukua jukumu la kuwatafutia watoto
hao shule badala ya kuwabebesha mzigo huo wazazi pamoja na walezi.
Wakizungumza
katika Ofisi za Tanzania Daima, wazazi hao walisema kuwa Novemba 27 mwaka huu
wakati shule zinafungwa walipokea barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji zikieleza
kwamba shule hiyo imefungwa hivyo wanaombwa kuwatafutia watoto wao nafasi kwenye
shule nyingine.
Wazazi
hao walisema kuwam, jukumu hilo si la kwao bali lilipaswa kufanywa na
halmashauri yenyewe kwani licha ya baadhi yao kujaribu kutafuta nafasi katika
shule nyingine lakini jitihada zinaonyesha kugonga mwamba kutokana na majibu
wanayoyapata kutoka kwa walimu wakuu wa shule hizo.
“Barua
inatuomba kuwatafutia watoto nafasi katika shule jirani ili msimu wa masomo
unapoanza January 2016 watoto wawe wameshapata shule lakini hili jukumu
limekuwa nzito kwetu kwa sababu kila shule tunazopita kutafuta nafasi,
tunaambiwa nafasi zimejaa,”alisema Rose Moris.
Aidha
katika hatua nyingine wazazi wa watoto hao kwa pamoja walisema kuwa ni vema
ofisi ya mkurugenzi ikachukua jukumu la kulisimamia na kulitekeleza suala hili
badala ya kuwaachia wazazi na walezi pekee yao.
“Ofisi
ya halmashauri ndio inapaswa kulitekeleza hili kwani wao ndio wamiliki wa shule
zote na ndio waajiri wa walimu hivyo kwao itakuwa ni rahisi tofauti na sisi
wazazi,”aliongeza mzazi.
Aidha,
katika hatua nyingine wazazi hao walionekana kuipongeza serikali kwa hatua
waliyoichukua ya kuikarabati upya shule hiyo ambayo ilijengwa tangu
utawala wa wakoloni hivyo majengo yake kuwa chakavu na yanayohatarisha
maisha ya watumiaji.
Hata
hivyo, barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCC/WD/U.21/9/VOL.1/12 ya tarehe
24/11/2015 kutoka halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenda kwa wazazi inaeleza
kuwa uamuzi wa kuifunga shule hiyo kwa ajili ya ukarabati mpya unatokana na
uchakavu mkubwa wa miundombinu ya shule hiyo ambayo ni madarasa,Ofisi,Vyoo, na
kwamba yanaweza kuporomoka wakati wowote.
Shule
hiyo ya Azimio inayo kadiriwa kuwa na wanafunzi zaidi ya 400 imefungwa kwa muda
usiojulikana huku kukiwa na taarifa kuwa Jijiji hilo lina mpango kuibadilisha
kuwa shule ya Mchepuo wa Kingeleza “English Medium”.
Akijibu
malalamiko hayo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Dkt Sammwel Lazaro alisema kuwa
waliamua kualicha jukumu hilo kwa wazazi wachagua shule wanazipenda na
zipo karibu na makazi na kwamba wale watakao kosa Halmashauri itachukua jukumu
la kuwatawanya katika shule zilizopo ndani ya jiji.
Akizugumzia
uaumizi wa kuibomoa shule hiyo Dkt Lazaro alisema wamefikia umauzi huo baada ya
wataalamu wa majengo kutoka jiji kujirisha kuwa jengo hilo kuwa la muda mrefu
hivyo halifai kwa matumizi ya binadamu kwa sasa.
'Ni
kweli shule inapaswa kufanyiwa ukarabati na majengo mengine yanatakiwa kujengwa
upya na hii baaada ya ya kupokea taarifa kutoka timu ya wataalamu ambao
walifika na kulifanyika uchunguzi jengo hilo ambao lilijengwa mwaka 1957 hivyo
na kuona kuwa halifai kwa matumizi ya binadamu' alisema Lazaro
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SHULE YA MSINGI AZIMIO YA BOMOLEWA KUPISHA UJENZI MPYA WA JENGO LA KISASA MBEYA ”
Post a Comment