Tuesday, March 25, 2014
SHUGULI ZA KUITAFUTA MH370 YASITISHWA.
Do you like this story?
Jamaa za abiria wa ndege hiyo wamekumbwa na majonzi makubwa. |
Mamlaka ya usalama wa safari za baharini nchini
Australia imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya shirika la Malaysia
iliyotoweka imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa na mawimbi makali
baharini.
Taarifa zinasema kuwa upepo mkali pamoja na mvua
kubwa inayonyesha katika eneo hilo ina maana kuwa ndege hazitoweza kupaa kwa
usalama. Mawimbi makali yameilazimisha meli ya jeshi la wanamaji wa Australia
kuondoka katika eneo ambalo mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege hiyo yalionekana
hapo jana Jumatatu.
Dr Erik van Sebille, ambaye ni mtaalam wa maswala
ya Baharini katika chuo kikuu cha New South Wales mjini Sydney, amefanya
utafiti katika eneo hilo la kusini mwa Bahari Hindi kutambua ni wapi na vipi
vifusi vinasafirishwa na mawimbi ya bahari. Anasema itakuwa vigumu sana kupata
mabaki ya ndege hiyo.
" Ni eneo lisiloweza kukalika duniani, acha
niseme. Upepo unaovuma ni mkali sana, mawimbi ni makubwa, ni mojawepo wa
mawimbi makubwa zaidi baharini.
Unapofika katika eneo hili la kusini, unaanza
kuhisi athari za eneo la Antactica kwenye bahari. Hapa tunazungumzia dhoruba
kali kali sana hususan wakati huu tunapoingia majira ya kupukutika,"
anasema Dr. Erik van Sebille.
Kadhalika amesema kuwa vifusi vilivyoenekana hapo
jana tayari vimekwishaondolewa katika eneo hilo na mawimbi makali.
"Haitakuwa rahisi kabisa kupata kijisanduku
cha kunasa habari. Mawimbi ya eneo hili ni makali na kwa hiyo vifusi ambavyo
wametambua kwa sasa huenda vimehamishwa katika kipindi cha majuma mawili au
matatu tangu ndege hiyo ianguka-na huenda vimesafiri kilomita alfu moja tayari.
Na hii inaifanya vigumu kurejelea utafutaji kwa sababu bahari inabadilika sana
hapa-ina vurugu ukipenda."
Hapo awali naibu waziri wa mashauri ya nchi za
Kigeni wa China Xie Hangsheng, aliitaka serikali ya Malaysia kutoka ushahidi
unaoelezea kuwa ndege hiyo ilianguka katika eneo la Kusini mwa bahari Hindi.
Ndege hiyo ilitoweka kwenye mtambo wa Radar zaidi ya majuma mawili
yaliyopita.Chanzo BBC Swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SHUGULI ZA KUITAFUTA MH370 YASITISHWA. ”
Post a Comment