Tuesday, March 25, 2014
SITTA AMKATAA WALIAOBA BUNGENI.
Do you like this story?
Jaribio la kutaka kumrejesha bungeni
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ili ajibu
masuala yaliyoibuliwa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya kufungua
Bunge limegonga mwamba.
Uamuzi wa kukataa ombi hilo
ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta wakati akijibu
mwongozo ulioombwa na Mjumbe wa Bunge, Julius Mtatiro, akisema hadhani kama ni
sahihi ombi hilo kutekelezwa.
Awali Mtatiro aliomba mwongozo kwa
mwenyekiti, akitaka kujua iwapo kuna haja ya kumrejesha Jaji Warioba kutoa
ufafanuzi juu ya baadhi ya hoja za Rais Kikwete ambazo zimekinzana na maoni ya
wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.
Mtatiro alisema: “Mtoa hoja mahususi
alikuwa ni Jaji Warioba na Rais Kikwete alialikwa kama mgeni rasmi kufungua
Bunge, lakini badala yake alikuja kujibu hotuba ya Warioba.
“Kwa sababu Rais alikaribishwa kama
mgeni rasmi, lakini alijibu hoja za Warioba, je, hatuoni kama kuna
haja ya kumrejesha mtoa hoja mahususi aje kujenga hoja kutokana na
alichosema Rais Kikwete?” alihoji Mtatiro ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa
CUF.
Katika ufafanuzi wake, Sitta alisema
tayari amepokea kwa maandishi kutoka kwa baadhi ya wajumbe kuzungumzia suala
hilo, jambo ambalo litafanyika lakini si kwa kumwita tena Jaji Warioba.
“Tunapenda kupata muda wa
kuzungumzia suala hili ili kuliweka sawa, hotuba zote mbili ambazo ni
muhimu zitaandaliwa ili kupitiwa kuona kama malalamiko yanayotolewa yana hoja,”
alisema Sitta.
Tangu Rais Kikwete ahutubie Bunge Ijumaa na
kutoa hoja kinyume na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba, hasa muundo wa Muungano,
kumeibuka mijadala ya ama kuipinga au kuiunga mkono, huku wengine wakieleza
kuwa imekiuka sheria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SITTA AMKATAA WALIAOBA BUNGENI.”
Post a Comment