Tuesday, March 25, 2014

MAHAKAMA: MTUHUMIWA KESI YA TWIGA AKAMATWE.




Mahakama imetoa amri ya kukamatwa ahmed ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi ya utoroshaji wa twiga wane kwenda uarabuni.

Hati ya kukamatwa  mshatikiwa huyo ilitolewa  jana na hakimu mkazi  mfawidhi wa mkoa  Kilimanjaro, simon kobelo baada ya mshtakiwa kushindwa  kufika mahakamani jana bila kutoa sababu.

Amri  hiyo inafuatia  ombi lililotolewa na wakili wa serikali evetha muchi  baada ya mshtakiwa  huyo  kutofika mahakamani kwa siku ya pili mfululizo.

Wakili huyo aliomba mahakama  itoe amri hiyo ili mtuhumiwa akamatwe  na kufikishwa mahakamani  leo na kama alikuwa ni mgonjwa awasilishe vyeti  kuthibitisha  ugonjwa wake.

Evetha alisema kitendo cha ahmed kutofika  mahakamani  bila kutoa sababu zozote  kimeisababisha serikali hasara kutokana na  na mawakili hao kusafiri kutoka dare s salaam hadi moshi.

Hakimu kobelo alikubaliana na ombi hilo la upande wa mashtaka na kuamuru  mshtatikiwa kukamatwa.

Mwenzi uliopita kesi hiyo ililazimika kuahirishwa baada ya mshatikiwa  kuugua ghafla muda mfupi kabla ya kesi hiyo inayowakabili pia watanzania watatu kuanza kusikilizwa.

Watuhumiwa wengine  ni hawa mang’unyuka, martin kimath na Michael mrutu ambao wote wako nje k kwa dhamana .

Wanyama waliotoroshwa  walikuwa na thamani y ash 170.5 milioni na walisafirishwa  kwa ndege kubwa ya jeshi la Qatar.

Ushahidi  wa awali mahakamani h apo unaonyesha kuwa wanyama  hao walikamatwa katika  maeneo yam to wa mbu.  Elboreti na engaruka wilayani monduli.

0 Responses to “MAHAKAMA: MTUHUMIWA KESI YA TWIGA AKAMATWE.”

Post a Comment

More to Read