Thursday, April 27, 2017
Maajabu ya Dunia… Binti Darasa la 7 Aota Matiti Manne
Do you like this story?
Ukistaajabu
ya Musa utayaona ya Firauni! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia
familia moja kukumbwa na mauzauza baada ya watoto wa mama aliyefahamika
kwa jina la Hawa Hassan Ngonyani kupatwa na mabadiliko ya maumbile
ambapo mmoja ameota matiti na mwingine kuanza kuotwa na uvimbe shingoni.
Hawa
anaishi na wanaye watatu maeneo ya Kinzudi Kata ya Goba, jijini Dar
ambapo waandishi wetu walifika na kujionea hali halisi ya watoto hao.
Mara
baada ya waandishi wetu kufika katika nyumba hiyo, walipokelewa na Hawa
aliyeonekana kukata tamaa ya maisha kutokana na jinsi anavyoishi kwa
malumbano na mumewe anayedaiwa kuitelekeza familia yake.
Akizungumza
na mwandishi wetu nyumbani hapo, Hawa alisema aliolewa ndoa ya mkeka
miaka kadhaa iliyopita huku mwanaume akimzalisha ‘fastafasta’.
Alisema
mwanaye mwenye umri wa miaka kumi na mbili anayesoma darasa la saba
katika Shule ya Msingi Kinzudi, alizaliwa mzima huku akiwa na chuchu
mbili tu hadi mwaka jana mwanzoni ndipo alipokumbwa na balaa hilo la
kuota chuchu zingine sehemu za juu ya titi za kawaida ambazo hadi sasa
zinazidi kukua siku hadi siku.
Akizidi
kufafanua, mama huyo alisema mara baada ya kuona hali hiyo, aliamua
kumshirikisha baba watoto wake ambaye ni kama amehama kabisa nyumbani,
lakini alikosa ushirikiano kwa mumewe huyo kwani hadi sasa mtoto
hajapelekwa hospitali kufanyiwa uchunguzi, kwani zile chuchu zinazidi
kukua pamoja na kumkosesha amani mtoto huyo anayejiandaa na mitihani ya
kuhitimu darasa la saba.
Hawa
alisema wakati akihangaika na mwanaye huyo wa kwanza namna ya kumpeleka
hospitali bila msaada, mtoto wake mwingine ameanza kuota uvimbe
shingoni ambao unahitaji jitihada za haraka kuutibu kabla haujawa
mkubwa.
Na alipomueleza tena mumewe, pia hakumpa ushirikiano.
“Yaani
alichonijibu ni kuwa yeye kwa sasa ana madeni mengi hivyo hana fedha,
nifanye michakato mingine nikawatibu yeye hana hela kwa sasa,” alisema
bi mkubwa huyo huku akibubujikwa na machozi.
Hata hivyo, dada huyo alisema mumewe ni mkorofi kwani pia amewahi kumpiga hadi kusaidiwa na majirani.
Mwanamke
huyo alihitimisha kuomba msaada kwa taasisi na mashirika ya utetezi wa
haki za binadamu wamsaidie kumuachanisha na mwanaume huyo ambaye pia
inadaiwa hutumia kilevi.
Hawa
alisema anahofia usalama wake kutokana na kupigwa mara kwa mara na
mbaya zaidi wakati anampiga huwa anamvua nguo zote na kumdhalilisha
mbele ya watoto hivyo kukimbilia kwa majirani akiwa mtupu.
Aidha,
pia mtoto huyo mwenye tatizo la kuota matiti ya ziada, alisema anaamini
manyanyaso ya kutopewa huduma na mama yake kudhalilishwa vinatokana na
mchepuko wa baba yake ambapo kuna siku alinasa mazungumzo live ya baba
yake akiongea na mchepuko wake, lakini kikubwa kinachomuuma ni kulala na
njaa au kunywa uji ambao hauna sukari.
Kufuatia
tuhuma hizo, gazeti hili lilimsaka baba wa watoto hao aliyefahamika kwa
jina la Abdul Liloka ili kuelezea kwa nini amekuwa akiinyima haki za
msingi familia yake na hapa anaelezea tuhuma hizo:
“Ndugu
mwandishi kwanza ni kweli mke wangu alinipatia taarifa za wanangu
kuumwa lakini hali ya Magufuli sasa ni ngumu, mimi nilikuwa na madeni
kibao ila kwa sasa nimemaliza nikipata hela nitampeleka hospitali huyu
mdogo mwenye uvimbe.”
Kuhusu
huyu mwingine mwenye matiti manne pia alisema: “Jamani hayo maziwa
yaliyoota huo ndiyo utamaduni wa familia yetu, wapo dada zangu wengi
wameota pia kwa hiyo hapo hamna tatizo tena bora hata yeye ni madogo
yupo shangazi yake mmoja anayo makubwa balaa.”
Alipoulizwa kuhusu tuhuma za kuitesa familia yake kutokana na kuwa na mchepuko, Liloka alisema:
“Jamani
mimi ni Muislam nina haki ya kuoa hata wanawake kumi si uwezo wangu, ni
kweli nina mchumba mwingine nje hata huyo aliyewapa taarifa kwa maana
ya mke wangu anamjua sana na kuhusu kumpiga ni kweli kuna siku nilimpiga
kofi moja tu!”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)