Friday, April 28, 2017

SURUALI CHAFU ZAGEUKA DILI..ZAUZWA DOLA 425


Wengi katika mitandao ya kijamii wameishutumu kampuni hiyo ya mavazi

Kampuni moja ya mavazi nchini Marekani imeshutumiwa vikali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutangaza kwamba inauza suruali za jeans zilizo na uchafu kwa $425 (£330; €390) sawa na zaidi ya 850,000 ya Tanzania.

Kampuni ya Nordstrom imezipa suruali hizo jina Barracuda Straight Leg.

Suruali hizo zimebandikwa matope yaliyokauka.

Jeans hizo zimeelezwa na mtandao wa Nordstrom kuwa kiashiria cha maisha magumu ya Wamarekani wafanyakazi na pia dhihirisho la kutia bidii kazini.

Lakini wakosoaji kwenye Facebook wamesema mavazi hayo ya kampuni hiyo yanasikitisha.

"Unaweza kupata sura sawa kwa kutumia pesa kidogo sana, kwa kujigaragaza kwenye shamba lako au kwenda shambani kulima na kupalilia mimea au maua," mmoja alisema.

Mtangazaji wa kipindi cha Dirty Jobs katika runinga ya Discovery Channel Mike Rowe amesema suruali hizo "zinaonekana kama zimevaliwa na mtu aliyefanya kazi yenye uchafu mwingi" lakini "zimeshonewa watu wasiogusa uchafu".Nordstrom imesema mavazi hayo yamepakwa matope maalum na kukaushwa

Nordstrom imesema mavazi hayo yamepakwa matope maalum na kukaushwa na lengo ni kuonyesha kwamba anayeyavalia hana wasiwasi wa kupata uchafu akifanya kazi yoyote  ile

 
. 
Mwezi jana Nordstrom walianza kuuza jeans zenye 'dirisha magotini'

"Nipe jeans zako kisha uniongezee dola 200, nitakuandalia vazi lako. Unaweza kuamua iwapo unataka uchafu wa kinyesi cha farasi au kuku, grisi kutoka kwenye trekta au udongo wa mfinyanzi... na kwa $600 nitampa mbuzi atafune jeans zako na kutoboa mashimo," aliandika mmoja wa wakosoaji.

Lakini kunao wengine waliosema iwapo kuna watu wanaoweza kulipa $400 kununua mavazi hayo machafu, basi nawalipe.

Mwezi jana Nordstrom walianza kuuza jeans zenye 'dirisha magotini' ambazo zinauzwa $95 (£74; €87) .

0 Responses to “SURUALI CHAFU ZAGEUKA DILI..ZAUZWA DOLA 425”

Post a Comment

More to Read