Friday, April 28, 2017
LIPUMBA: KUNA MATUKIO YANAPANGWA NJE YA CHAMA CHA CUF ILI KIFUTWE KWA VURUGU
Do you like this story?
“Baada ya kulisikia hilo niliamua kuchukua jukumu la kuwaandikia Jukwaa
la wahariri barua ambayo ipo mbioni kwenda kwenye ofisi zao kwamba mimi
binafsi kama mwenyekiti wa CUF nalaani kitendo cha kupigwa kwa waandishi
wa habari na ni jambo ambalo hatulikubali kabisa, hatuwezi kujenga
Demokrasia ikiwa waandishi wa habari hawafanyi kazi yao katika hali ya
amani na utulivu”.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF anayetambulika na ofisi ya msajili
wa vyama vya siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amesema ameandika barua
maalumu kwa jukwaa la wahariri kuonesha kusikitishwa kwake na vurugu
zilizotokea hivi karibuni katika mkutano wa CUF na kusababisha waandishi
kufanyiwa fujo.
Prof Lipumba ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio
hilo ameyasema hayo katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Azam Two
na pamoja na mambo mengine amemtaka katibu mkuu wa CUF Maalim Seif wakae
wazungumze ili wamalize tofauti zao na wakae wakijenge chama..
“Vile vile kijana wetu amekatwa kisigino kwa panga na anavyo elewa yeye
kijana aliyemkata anaitwa Mohamedi Mgonvi na taarifa hii imepelekwa
kwenye vyombo vya dola kwa hiyo vyombo vya dola vinalishughulikia na
tulitoa wito ambao ulitolewa na Mkurugenzi wetu wa habari na uenezi”
“Mimi toka awali nimeeleza kwamba nataka tumalize tofauti za kisiasa kwa
mazungumzo tupate suluhu tuheshimu katika ya chama chetu na nimekuwa
nikimuita Maalim Seif aje ofisi bugurudi aweze kuzungumza afanye kazi
zake kama katibu mkuu na mimi nimemfahamu Maalim Seif mwaka 1973 tukiwa
wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam kwahiyo hatuna sababu ya sisi kuwa
na mgogoro huu na kuuruhusu kuendelea”
“Hivi sasa kupitia taarifa zetu za kiuchunguzi zinaonesha kwamba kuna
mbinu ya kutaka chama hiki kiweze kufutwa kwa hiyo kuna matukio
yanapangwa nje ya chama ili paweze kutokea vurugu na zikishatokea waseme
chama hiki hakifai kuendelea kuwa chama cha siasa na utakuta kuna vyama
vingine vya siasa vinashabikia na kutoa wito ili chama hiki kiweze
kufutwa” Prof. Lipumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LIPUMBA: KUNA MATUKIO YANAPANGWA NJE YA CHAMA CHA CUF ILI KIFUTWE KWA VURUGU”
Post a Comment