Sunday, July 10, 2016
SHULE YA SEKONDARI LINDI YAUNGUA MOTO.
Do you like this story?
Shule
ya Sekondari ya Lindi imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo tarehe
10/07/2016. Moto huo ambao ulianza majira ya saa saba usiku na uliweza
kudhibitiwa kutoleta athari zaidi baada ya Jeshi la Polisi, Zimamoto na
Wananchi kushirikiana kwa pamoja na kufanikiwa kuudhibiti saa moto asubuhi leo.
Mpaka
moto huu ulipodhibitiwa mali zifuatazo zilikuwa tayari zimeshaungua:-
Madarasa
tisa yameungua,ambapo matano yameungua pamoja na samani zilizokuwa ndani na
mengine manne ni majengo peke yake Vifaa viliwahi kuokolewa na wananchi.
Ofisi
nne za walimu.
Maabara
mbili za kemia na fizikia zimeungua kwenye paa tu, hivyo samani za ndani
hazijaungua.
Takribani
madawati zaidi ya 300 yameteketea kwa moto.
Majengo
mengine ya shule yapo salama yakiwemo mabweni. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe.
Godfrey Zambi amewaomba wananchi na uongozi wa shule kuwa watulivu wakati
Uongozi wa Mkoa ukitafuta namna ya kusaidia Wanafunzi kuendelea na mafunzo
baada ya kufunguliwa kwa Shule hiyo kesho tr 11/07/2016
Aidha,
Mkuu wa Mkoa amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kuuzima moto huo kwani
haikuwa kazi rahisi, pia amewashukuru polisi na jeshi la zimamoto kwa jitihada
walizochukua katika kuudhibiti moto huo.
Kwa
sasa inafanyika tathmini ya mali zilizoteketea kutokana na moto huo sambamba na
uchunguzi wa chanzo cha moto. Taarifa kamili ya uchunguzi na tathmini itatolewa
pindi itakapokamilika.
Katika
Hatua Nyingine Mtu Mmoja alietaka Kuiba Laptop katika tukio hilo amekamtwa na
Polisi baada ya Wananchi kuanza kumpa Adhabu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SHULE YA SEKONDARI LINDI YAUNGUA MOTO.”
Post a Comment